top of page

Kamusi Tiba ya ULY CLINIC

Pituitary ni nini?

Pituitary

Ni tezi inayofahamika kiswahili kama Pituitari ambayo ni tezi ndogo iliyopo kwenye msingi wa ubongo ambayo inadhibiti utoaji wa homoni mbalimbali muhimu kwa kazi za mwili. Mara nyingi huitwa “tezi mama” au kwa sababu inadhibiti au kuchochea tezi nyingine za mfumo wa homoni kufanya kazi zake.

Compound ni nini?

Compound

Kampaundi au molekyuli ni kijenzi cha kemikali kinachoundwa na atomi moja au zaidi zinazoungana kwa muundo maalumu. Katika mwili, kijenzi hiki huchangia mchakato wa metabolism, ikijumuisha kuvunjwa kwa baadhi ya kijenzi kupata nishati au kutengeneza misombo muhimu kwa seli na tishu.

Metabolism ni nini

Metabolism

Umetaboli ni mchakato wa kikemikali unaotokea ndani ya mwili unaoruhusu seli kuchakata chakula kuwa nishati, protini, mafuta, na kampaundi muhimu. Mchakato huu pia husaidia mwili kuondoa taka, kudumisha viwango vya nishati, na kudhibiti shughuli za seli.

Growth Hormone ni nini?

Growth Hormone

Growth hormone hufahamika kiswahili kama Homoni ya Ukuaji, ni homoni inayozalishwa na tezi ndogo ya pituitari na ambayo ina jukumu la msingi katika ukuaji wa mifupa, misuli, na tishu nyingine mwilini. Homoni hii pia inachangia udhibiti wa umetaboli wa mafuta, protini, na sukari.

CD4 ni nini?

CD4

CD4 ni seli za kinga zinazosaidia mwili kujilinda dhidi ya magonjwa. Kadiri idadi ya CD4 inavyopungua, ndivyo kinga ya mwili inavyokuwa dhaifu.

bottom of page