top of page

Kamusi Tiba ya ULY CLINIC

Kitovu cha mtoto

Kitovu cha mtoto

Kitovu cha mtoto ni nini?

Kiunga mwana

Kiunga mwana

Ni mkusanyiko wa mishipa ya damu ya vena na arteri iliyofunikwa kwa pamoja na kuta ya tishu na hivyo kuifanya iwe na mwonekano wa kamba nyeupe inayoteleza.

Kiwango cha chini cha kolestero nyepesi kwenye damu ni nini?

Kiwango cha chini cha kolestero nyepesi kwenye damu

Pia kama kiwango cha chini cha lehemu nyepesi ni hali ambapo kiwango cha LDL (lipoproteini yenye msongamano mdogo) katika damu huwa chini kuliko kiwango kinachotarajiwa. LDL hubeba kolestero kutoka kwenye ini kwenda kwenye sehemu mbalimbali za mwili.

Kiwango cha chini cha koletroli nzito kwenye damu ni nini?

Kiwango cha chini cha koletroli nzito kwenye damu

Ni hali ambapo kiwango cha Kolestro nzito katika damu huwa chini kuliko kiwango kinachotarajiwa. Kolestro nzito husaidia kubeba kolesteroli kutoka kwenye mishipa ya damu kwenda kwenye ini, ambako inaweza kuchakatwa na kuondolewa mwilini.

Kiwango cha juu cha kolestro nyepesi kwenye damuni nini?

Kiwango cha juu cha kolestro nyepesi kwenye damu

Ni hali ambapo kiwango cha Lehemu nyepesi (low-density lipoprotein) katika damu huwa juu kuliko kiwango kinachopendekezwa. Lehemu nyepesi hubeba kolestroli kwenda kwenye tishu za mwili, lakini ikiwa iko nyingi inaweza kujikusanya kwenye kuta za mishipa ya damu na kutengeneza mabonge ya mafuta yanayoweza kupunguza au kuziba mtiririko wa damu.

bottom of page