top of page

Kamusi Tiba ya ULY CLINIC

Motor Agraphia ni nini?

Motor Agraphia

Hufahamika kiswahili kama Agrafia ya misuli, ni aina ya agrafia inayotokea pale ambapo mtu hushindwa kuandika kwa usahihi kutokana na udhaifu wa misuli, kupooza, au matatizo ya neva yanayodhibiti harakati za mkono na vidole. Katika hali hii, mfumo wa lugha huwa haujaathirika; mtu anaweza kufikiri, kuelewa, na kupanga maneno kwa usahihi, lakini hushindwa kuyatekeleza katika maandishi kwa sababu ya changamoto za kimwili.

Msamba (periniamu)ni nini?

Msamba (periniamu)

Msamba (periniamu) ni eneo la mwili lililopo kati ya sehemu za siri na njia ya haja kubwa. Kwa mwanamke, msamba huanzia kwenye sehemu ya chini ya mlango wa uke na kuendelea hadi kwenye njia ya haja kubwa. Kwa mwanaume, eneo hili hupatikana kati ya mfuko wa korodani na njia ya haja kubwa.

Mshituko wa sepsisi

Mshituko wa sepsisi

Mshituko wa sepsisi ni hatua kali ya sepsisi ambapo shinikizo la damu hushuka sana na viungo muhimu vya mwili hupata damu ya kutosha kwa shida. Ni dharura ya kitabibu inayohitaji matibabu ya haraka ili kuokoa maisha.

Mtafunokinga

Mtafunokinga

Hutokea endapo mwili unazalisha chembe ulinzi zinazoshambulia chembe zingine hai za mwili, mfano wa magonjwa ya mtafuno kinga ni baridi ya bisi.

Muingiliano wa dawa

Muingiliano wa dawa

Ni mwingiliano unaotokea endapo dawa moja imetumika pamoja na nyingine kuweza kusababisha dawa hizo zisifanye kazi kama ilivyokusudiwa.

bottom of page