top of page
Kamusi Tiba ya ULY CLINIC
Takikadia
Ni hali ambapo moyo hupiga kwa kasi zaidi ya kawaida, yaani mapigo ya moyo ya mtu mzima aliyepumzika yanazidi 100 kwa dakika. Takikadia ni jina la kitabibu linalotumika kuelezea mapigo ya moyo kwenda kasi. Kwa kawaida, mapigo ya moyo ya mtu mzima aliyepumzika huwa kati ya 60–100 kwa dakika.
bottom of page

