Unaweza bofya ili kusoma zaidi kuhusu huduma ya kwanza kwenye mada hizi;
Imeandikwa na daktari wa ULY Clinic
​
Kupaliwa
​
​
Endapo hali ya kupaliwa si mbaya ikiwa inamanisha kuwa njia ya hewa halijazibwa kikamilifu, aliyepaliwa atakuwa na uwezo wa kuongea, kulia, kukohoa na kupumua
Kwenye hali kama hii, aliyepaliwa mara nyingi huweza kusafisha fumo wa hewa kwa kukohoa tu.
​
Endapo hali ya kupaliwa si mbaya fanya yafuatayo
​
-
Muhimize aliyepaliwa kukohoa zaidi na kwa nguvu ili kuzibua njia ya hewa
-
Mwambie aliyepaliwa ajalibu kutema kilichompalia kama kipo mdomoni
-
Usiweke kidole kwenye mdomo kama huoni kilichompalia, ukifanya hivyo utasababisha kukisukuma ndani zaidi na kufanya hali ya kupaliwa kuwa mbaya
-
Kama kukohoa hakutasaidia anza kutumia kiganja cha mkono kumpiga mgongoni
​
Hali mbaya ya kupaliwa
​
Endapo aliyepaliwa ana hali mbaya, atakuwa na dalili za kutokuwa na uwezo wa kuongea, kulia, kukohoa au kupunua, bila msaada wowote mtu huyu atapoteza fahamu au kuzimia
Ili Kumsaidia mtoto au mtu mzima mwenye umri Zaidi yam waka 1 fanya yafuatayo;
-
Kaa nyuma yake, kwa upande mmoja kiasi. mlaze kifua chake kwenye mkono wako mmoja. Mwegamishe kwenye huu mkono mmoja na hapo kilichoziba njia kitatoka mdomoni kuliko kuendelea kwenda chini ya mfumo wa hewa
-
Mpige kwa nguvu hadi mara tano katikati ya mabega kwa kutumia kisigino cha mkono( kisigino cha mkono ni eneo kati ya kiganja na kifundo cha mkono)
-
Tizama endapo kilichoziba hewa kimetoka na njia imefunguka
​
Kama sio tumia njia ya kubana tumbo kwa mikono miwili
​
Ili kuweza kufanya shughuli hii ya kumsaidia aliyepaliwa fanya yafuatayo;
-
Kaa nyuma yake
-
Weka mikono yako kwenye maeneo ya nyonga na mkunje kiasi kuelekea mbele
-
Kunja ngumi moja na ikae karibu na kitovu
-
Weka mkono mwingine juu ya hiyo ngumi kisha kandamiza ngumi kuelekea ndani na juu kwa kutumia nguvu na kwa haraka
-
Usitumie nguvu kupita kiasi
-
Rudia hivyo mara tano
​
Madhumuni ya shughuli hii ni kuzibua njia ya hewa kwa kila tendo utalofanya.
​
Kama njia bado imeziba licha ya kujaribu mambo yote matano
​
-
Piga simu 112 ili gali la mahututi lije mchukua
-
Endelea na mizunguko mingine ya kujaribu kuzibua njia kama maelekezo yanavyoosema hapo juu
​
Mtu aliyepaliwa siku zote anatakiwa aonanae na mtaalamu wa afya siku zote hata baada ya njia kufunguka ili achunguzwe endapo amepata jeraha au kuna kipande cha kitu kilichompalia kimebaki kwenye njia ya hewa.
ULY CLINIC inakushauri siku zote ufuate ushauri wa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote inayohusu afya yako.
​
​
​
Tufahamishe kingine unachotaka kujua kwa kuandika maoni yako katika blogi yetu na foramu
​
Imeboreshwa mara ya mwisho 17.03.2020