top of page
Unaweza bofya ili kusoma zaidi kuhusu huduma ya kwanza kwenye mada hizi;
Huduma ya kwanza kwa mtu aliyeungua
Imeandikwa na ULY CLINIC
Kama mtu ameungua na moto maeneo ya nje ya mwili ni vema kufanya yafuatayo;
Pooza eneo lililoungua haraka iwezekanavyo kwa maji ya baridi (maji ya bomba) kwa angalau muda wa dakika 30 na kuendelea, mpaka maumivu yaishe
Unaweza kutumia maji ya bomba yanayotiririka au kumwagia maji sehemu iliyoungua kwa mwendelezo
Piga simu 112 kutafuta ushauri wa kitaalamu wakati unaendelea kupoza kidonda kwa umakini.
bottom of page