top of page

Kudhuriwa na sumu

Imeandikwa na madaktari wa uly clini

Kudhuriwa na sumu kunaweza kumsababisha mtu apoteze uhai

Mara nyingi kudhuriwa na sumu husababishwa na mtu mwenyewe kunywa sumu kama vile mtu kunywa dawa nyingi kupita dozi aloandikiwa, kula uyoga na baadhi ya mimea.

Dalili za kudhuriwa na sumu kutokana na kunywa kiwango kikubwa cha pombe huweza sababisha dalili zinazofanana na mtu aliyekunywa sumu

Madhara?dalili za kudhuriwa na sumu hutegemea aina ya sumu mtu aliyotumia lakini huwa pamoja na hizi zifuatazo

Kutapika, kupoteza fahamu, maumivu au hisia za kuungua n.k

Ushauri ufuatao ni muhimu sana kwa anayetoa msaada kwa mtu aliyedhuriwa na sumu

  • Tafuta kujua ni sumu gani iliyomdhuru ili uweze kumwambia daktari au mhudumu wa afya

  • Usimpe kitu chochote cha kula au kunywa isipokuwa tu umepata ushauri wa mhudumu wa afya au daktari

  • Usijaribu kumfanya atapike (kumtapisha), matapishi yanaweza kuingia kwenye mfumo wa hewa na kumuua

  • Kaa na huyu mtu kwa karibu sana kwa sababu hali yake inaweza badilika na kuwa mbaya au kupoteza fahamu, ukiwa karibu unaweza kutoa msaada wowote

 

Kama amepoteza fahamu wakati unasubiri msaada ufike tazama kama anapumua na ikiwa kuna ulazima fanya CPR.

Usiweke kinywa kwenye mdomo kwa mtu aliyedhuriwa na sumu sababu unaweza dhurika na sumu hii pia endapo imebaki mdomoni kwake.

Usimwache mwenyewe kwani anaweza kutapika kisha kupaliwa na sumu, hatimaye hali huwa mbaya zaidi

Kama akitapika, hifadhi matapishi kwa ajili ya kuwapa  wataalamu wa afya, yanaweza kuwasaidia kutambua aina ya sumu na kufanya matibabu ya kunasua sumu husika.

Kama aliyedhurika anajitambua na anapumua muweke katika pozi la kupona

Toleo la 3

Imeboreshwa, 21/12/2018

Unaweza bofya ili kusoma zaidi kuhusu huduma ya kwanza kwenye mada hizi;

 

Kupaliwa

Aliyevunjika

Namna ya kufanya CPR

Kung'atwa nyoka

Aliyezama maji

Kuungua

Kupigwa shoti

Shambulio la moyo

Dhuriwa na sumu

bottom of page