Imeandikwa na daktari wa ULY clinci
Magonjwa ya moyo na kiharusi
Watu wenye kisukari wapo kwenye hatari kubwa ya kupata magonjwa ya moyo na kiharusi, kwa jina jingine ikifahamika kama magonwa ya mishipa ya moyo na ubongo.
Mgonjwa wa kisukari anawez kupatwa na magonjwa ya moyo miaka 10 au 15 mapema zaidi ukilinganisha na mtu asiye na kisukari
Ugonjwa wa mishipa ya damu ya moyo(coronary artery) huongeza kwa kutokea kama ugonjwa wa moyo. Hutokea pale mishipa hii inapokuwa inapungua kizio (kupungua kwa ukubwa wa tundu ka mshipa wa damu) cha ndani na kupelekea kutofika kwa damu sehemu zingine za moyo kwa sababu damu haipiti ya kutosha au haipiti kabisa. Kupungua kwa kizio kunaweza kutokana na kuganda kwa mafuta(rehamu) ndani ya mishipa ya damu. Tendo hili huitwa “kuganda kwa mishipa ya ateri” kama mishipa ya damu inayolisha ubongo itaganda basi mtu anaweza kupata kiharusi.
Kiwango kikubwa cha sukari katika damu ni kihatarishi kimojawapo cha kupata kiharusi, lakini watuwenye kisukari huwa na vihatarishi vingine ambata. Vihatarishi hivyo vinahusisha uzito mkubwa kuputa kiasi(na haswa kwa mtu mwenye mafuta mengi maeneo ya kiunoni), kutoshughulisha mwili, shinikizo la juu la damu, na kuwa na kiwango cha juu cha rehani kwenye damu. Watu wanaovuta sigara au wenye historia kwenye familia ya kuwa na kiharusi au magonjwa ya moyo huonekana kuwa na wana kiharatishi kikubwa cha kupata magonjwa ya mishipa ya damu na ubongo.
Kupunguza Vihatarishi
Habari njema ni kwamba watu wenye kisukari wanaweza kupunguza vihatarishi vya magonjwa ya moyo na kiharusi kwa kuzingatia na kuweka umakini kwenye vihatarishi walivyonavyo. Kushirikiana na timu yako ya tiba kufikia malengo yafuatayo yataweza kukusaidia kudhibiti sukari na magonjwa ambata. Kupata uzito wa kiafya ,kula vyakula vyenye afya bora na kuushughulisha mwili kwenye mazoezi ni muhimu. Watu wenye wenye kisukari huweza kuhitaji nyongeza ya dawa ili waweze kufikia malengo hayo
Unafahamu kuhusu ABCDEs?
Ni kifupisho cha vitu unavyotakiwa kuzingatia au kufanya ili kupunguza vihatarishi vya magonjwa ya moyo na kiharusi. Mchanganuo umefanyikahapo chini kuhusu ABCDEs kwa kila herufi
A-A1C- lengo la A1C liwe asilimia 7%* au pungufu (AIC imeelezewa kwenye kitabu hiki hivyo fanya rejea)
B- Dhibiti shinikizo la damu( liwe pungufu ya 130/80*)
C- Cholesterol/rehamu ainaya LDL(rehamu mbaya) kiwango kiwe 2*mmol/L au pungufu
D- Dawa za kulinda moyo. Madawa ya kutibu shinikizo la damu la juu jamii ya ACE au ARBs, dawa za kupunguza rehamu mbaya kwenye damu, aspirini au clopidogrel. Ongea na daktari wako kuhusu madawa haya ya kukuzuia na kisukari pamoja na kiharusi ili upate ushauri.
E- Mazoezi.Mazoezi endelevu, kuushughulisha mwili, pamoja na chakula bora. Zingatia uzito unaoshauriwa kutokana na mwili wako*
S- Sigara na msongo wa mawazo/stress – acha kuvuta sigara na kabiliana na msongo wa mawazo ipasavyo
* Ongea na mtaalamu wako wa afya ili akushauri kiwango halisi kwako. Kumbuka malengo ya kiwango cha A1C ya mwanamke mjamzito, watoto wenye umri chini ya miaka 12 na mzee huwa tofauti tofauti.
Mwisho unaweza kuongea na daktari wako kuhusu mambo haya unayoshauriwa na namna ya kufikia malengo.
Madhara katika macho
Matatizo katika retina ya jicho sehemu inayopokea mwanga unaoingia katika jicho matatizo haya hutokana na uzalishaji wa mishipa ya damu mingi kupita kiasi, matokeo yake ni kuziba sehemu hii ya jicho na kusababisha dalili za kuona ukungu au kushindwa kuona. Tatizo hili linaweza kusababishwa na magonjwa mengine kama shinikizo la damu la juu.
Baada ya miaka 10 ya kuwa na kisukari, nusu ya wagonjwa hupata udhaifu katika retina unaosababisha kushindwa kuona, zaidi ya asilimia 80 ya wagonjwa wa kisukari watapata tatizo hili ndani ya miaka 15 ya kuwa na ugonjwa wa kisukari.
Tatizo hili huweza kupelekea kupungua uwezo wa kuona au kutoona kabisa kusikotibika kwa sababu ya kunyofoka kwa retina katika sehemu yake kwenye jicho.
Matibabu
Matibabu ya mwanga wa laser, huharibu tishu zilizozalishwa kwa wingi na kujikusanya katika retina na kupelekea kutoona, matibabu haya husaidia kuingia kwa hewa safi ya oksijeni kwenye retina na kuona vizuri.
Kumbuka matibabu haya yanatakiwa kufanyika mapema kabla retina ya jicho haijafunikwa kabisa.
Wasiliana na daktari wako siku zote kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatu yoyote
Imeboreshwa 12.03.2020