Kubadilika rangi ya ulimi kunaweza kusababishwa na kula chakula chenye rangi, maambukizi au upungufu wa vitamin aina fulani mwilini. Kila aina ya rangi inaweza kumaanisha tatizo aina fulani.
Maumivu ya ulimi yanaweza kusababishwa na hali au matatizo mbalimbali, maumivu yanaweza kuwa ya aina tofauti mfano kuhisi ulimi unawaka moto au kuchoma choma unapokuwa unakula au kunywa n.k.