top of page

Magonjwa na saratani mbalimbali

Sehemu hii utasoma kuhusu hali na magonjwa mbalimbali

Mapunye (tinea capitis)

Mapunye (tinea capitis)

Mapunye (tinea capitis), yanayojulikana pia kama vibarango, ni maambukizi ya fangasi wa ngozi ya kichwa na nywele, yanayoleta mabaka ya magamba, nywele kukatika na upara wa muda, na wakati mwingine uvimbe wenye usaha (kerion). Huwapata zaidi watoto lakini pia watu wazima. Huambukiza kupitia vitana, kofia na vinyozi. Hutibiwa kwa vidonge vya fangasi, si krimu peke yake.

Maambukizi ya njia ya mkojo (UTI)

Maambukizi ya njia ya mkojo (UTI)

Maambukizi ya njia ya mkojo (UTI) ni maambukizi ya bakteria kwenye kibofu, mrija wa mkojo au figo. Huleta kuungua wakati wa kukojoa, kukojoa mara kwa mara na maumivu ya tumbo la chini; homa na maumivu ya kiuno huashiria figo kuathirika. Wanawake huathirika zaidi. Hutibika kwa antibiotiki sahihi baada ya kipimo cha mkojo.

Maambukizi ya bakteria Helicobacter pylori

Maambukizi ya bakteria Helicobacter pylori

Helicobacter pylori (H. pylori) ni bakteria anayeishi kwenye utando wa tumbo. Zaidi ya nusu ya watu Afrika wanaye, wengi bila dalili, lakini kwa baadhi huleta uvimbe wa tumbo, vidonda vya tumbo na, mara chache, saratani ya tumbo. Hutambuliwa kwa kipimo cha kinyesi au pumzi na hutibiwa kwa mchanganyiko wa dawa kwa siku 14.

Maumivu sugu ya kibofu cha mkojo (interstitial cystitis)

Maumivu sugu ya kibofu cha mkojo (interstitial cystitis)

Maumivu sugu ya kibofu cha mkojo (interstitial cystitis au bladder pain syndrome) ni hali ya muda mrefu ya maumivu au shinikizo kwenye kibofu na nyonga, pamoja na kukojoa mara kwa mara na hamu kubwa ya kukojoa – bila maambukizi. Huwapata zaidi wanawake. Haina tiba moja; hudhibitiwa kwa mtindo wa maisha, mazoezi ya kibofu, dawa na tiba za kibofu.

bottom of page