top of page

Magonjwa na saratani mbalimbali

Sehemu hii utasoma kuhusu hali na magonjwa mbalimbali

Uvimbe kwenye kizazi: Visababishi, Dalili, Vipimo na Matibabu

Uvimbe kwenye kizazi: Visababishi, Dalili, Vipimo na Matibabu

Uvimbe ndani ya kizazi ni neno la jumla linalojumuisha magonjwa mbalimbali yanayosababisha ukuaji usio wa kawaida wa tishu ndani ya mji wa mimba, yakiwemo faibroidi, polipu za endometriamu, ukuaji wa endometriamu kupita kiasi na saratani ya endometriamu. Uchunguzi wa mapema, vipimo sahihi na matibabu yanayolingana na aina ya uvimbe ndiyo msingi wa kulinda afya ya uzazi na kuboresha matokeo ya matibabu.

Uvimbe Faibroidi: Dalili, Visababishi, Matibabu na Kinga

Uvimbe Faibroidi: Dalili, Visababishi, Matibabu na Kinga

Ni ugonjwa wa kawaida sana kwa wanawake na mara nyingi si saratani. Ingawa wanawake wengi hawapati dalili, wengine wanaweza kupata hedhi nyingi, maumivu makali, upungufu wa damu na matatizo ya uzazi. Uchunguzi wa mapema na matibabu yanayofaa husaidia kupunguza madhara na kuboresha ubora wa maisha. Mwanamke mwenye dalili zisizo za kawaida anatakiwa kufika kituo cha afya kwa uchunguzi badala ya kutegemea dawa ambazo hazijathibitishwa kisayansi.

Salmonellosisi

Salmonellosisi

Ni maambukizi ya bakteria Salmonella yanayoenezwa zaidi kupitia chakula au maji yenye vimelea, hasa mayai, kuku na nyama isiyoiva vizuri, na huanza kwa dalili zinazofanana na taifodi kama homa, maumivu ya tumbo, kuharisha na kutapika. Kwa watu wengi hupona ndani ya siku chache kwa matibabu saidizi, lakini watoto, wazee, wajawazito na watu wenye kinga dhaifu wako kwenye hatari ya kupata matatizo makubwa. Kuivisha chakula, kutumia maji salama, kunawa mikono kwa sabuni na kuwahi kupata huduma za afya endapo dalili ni kali au zinaendelea ni njia bora za kuzuia na kupunguza madhara yake.

Homa ya Matumbo: Dalili, Visababishi, Vipimo na Matibabu

Homa ya Matumbo: Dalili, Visababishi, Vipimo na Matibabu

Homa ya matumbo ni ugonjwa wa bakteria unaosambaa hasa kupitia chakula na maji yenye vimelea, na unaweza kuathiri mwili mzima endapo hautatibiwa mapema. Usafi wa mazingira, matumizi ya maji salama, uchunguzi wa mapema na matibabu sahihi ni nguzo muhimu za kuzuia madhara na kuzuia kuenea kwa ugonjwa huu.

bottom of page