top of page

Mwandishi:

Dkt. Mangwella S, MD

Mhariri:

Dkt. Salome A, MD

9 Julai 2023 17:44:57

Manii huishi kwa muda gani kwenye kizazi?

Je, mbegu za mwanaume ume hukaa masaa mangapi kwenye kizazi cha mwanamke?

Manii huishi kwa wastani wa muda wa siku 3, na ikiwa mazingira ni rafiki idadi ya siku zinaweza kuongezeka kufikia 5 kwenye kizazi cha mwanamke. Wakati huu endapo yai la mwanamke litatoka kwenye ovari linaweza kurutubishwa na kuanzisha safari ya ujauzito.


Baadhi ya tafiti zilizofanyika kwa wanawake zinaonyesha manii kuishi hadi kufikia siku 9 ukeni na zingine kufikia siku 12 katika shingo ya kizazi. Tafiti hazijaonyesha kama mbegu hizi zilizoishi muda mrefu bado zinakuwa na uwezo wa kuchavusha yai.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

9 Julai 2023 19:50:03

Rejea za mada hii

  1. Morrison AI. Persistence of spermatozoa in the vagina and cervix. Br J Vener Dis. 1972 Apr;48(2):141-3. doi: 10.1136/sti.48.2.141. PMID: 5032772; PMCID: PMC1048291.

  2. Clubb E. Natural methods of family planning. J R Soc Health. 1986 Aug;106(4):121-6. doi: 10.1177/146642408610600402. PMID: 3091823.

bottom of page