Mwandishi:
Dkt. Mangwella S, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
21 Oktoba 2021, 19:20:37
Tinidazole inatibu gono?
Hapana!
Licha ya kuwa miongoni mwa dawa za kutibu magonjwa ya zinaa, tinidazole hutumika kwenye matibabu ya ugonjwa wa trichomoniasis tu na haina uwezo wa kutibu gono.
Tinidazole inatibu nini?
Tinidazole ikifahamika kwa jina jingine la kibiashara kama Tindamax ni dawa jamii ya nitroimidazole hutumika kama yenyewe au ikiwa imeunganika na dawa zingine katika matibabu ya magonjwa yafuatayo;
Trichomoniasis (miongoni mwa ugonjwa wa ziaa)
Amibiasis au amiba
Giardiasis
Watu wengi huchanganya kati ya gono na magonjwa ya zinaa kwa sababu hudhani kutokwa na usaha ni gono. Gono ni moja ya ugonjwa wa zinaa unaoweza kusababisha kutokwa na usaha sehemu za siri.
Matibabu ya kutokwa na usaha sehemu za siri hulenga kutibu magonjwa ya zinaa na si gono tu hivyo ndo maana hutapewa dawa tinidazole tu katika matibabu ya magonjwa ya zinaa bali pamoja na dawa zingine.
Wasiliana na daktari kabla ya kutumia tinidazole na kama una gono, wasiliana na mtaalamu wa afya mwenye uzoefu na matibabu ya magonjwa ya zinaa ili upatiwe matibabu na kuepuka usugu wa vimelea kwenye dawa.Kutumia dawa pasipo ushauri husababisha vimelea kuwa sugu kwenye dawa hiyo na kutopona.
Rai
Epuka usugu wa vimelea wa maradhi kwenye dawa hii kwa kuitumia dawa baada ya kushauriwa na daktari tu.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
21 Oktoba 2021, 19:20:37
Rejea za mada hii
Lopez Nigro MM, et al. Genotoxicity and cell death induced by tinidazole (TNZ). Toxicol Lett. 2008 Jul 30;180(1):46-52. doi: 10.1016/j.toxlet.2008.05.017.
Fung HB, et al. A nitroimidazole antiprotozoal agent. Clin Ther. 2005 Dec;27(12):1859-84.
Drugbank. Tinidazole. https://go.drugbank.com/drugs/DB00911. Imechukuliwa 21.10.2021