top of page
Writer's pictureDr.Sospeter Mangwella, MD

Jinsi ya kutumia dawa ya kupuliza kutibu asthma


Pumu ya kifua ni hali ambayo njia za mfumo wa hewa/mfumo wa upumuaji huvimba na kuzalisha ute ute wa utelezi kupita kiasi. Hali hii huweza kusababisha kushindwa kupumua vema, kukohoa, miruzi katika kifua na kuishiwa pumzi.

Kwa baadhi ya watu, pumu huwa si tatizo sana kwao ikiwa na maana huwa haileti dalili za kutisha. Lakini kwa watu wengine wenye pumu huambatana na dalili kali zinazoweza kupunguza ubora wa amaisha yake

Pumu huwa haitibiki, lakini dalili zake zinaweza kutibiwa. Na kwa sababu pumu ya kifua hubadilika badilika mda hadi mda, ni vema kuongea na daktari wako ili aulize kuhusu dalili zako na afanye matibabu kulingana na dalili ulizonazo wakati husika.



Katika eneo hili ni vema ukajua njia sahihi ya kutumia dawa za pumu pale unapokuwa umeshikwa na dalili zake kwa ghafla


Dawa aina ya salbutamol inhaler inayoweza kuwa imechanganywa na aina nyingine kama corticosteroid(kwa baadhi ya watengenezaji hutengenezwa zikiwa zimechanganywa tayari) hutumika katika kupunguza dalili za pumu zinazoamka ghafla. Dawa hii endapo itatumika kwa usahihi itaweza kumwokoa mgonjwa wa pumu ya kifua


Hatua za utumiaji wa dawa hii ni hizi

  1. vuta hewa iingie ndani ya mapafu kwa jinsi uwezavyo kisha itoe nje ya mapafu yote kwa kupumua

  2. Kisha usivute hewa nyingine

  3. weka kikopo cha dawa yako katika mdomo haraka na bonyeza dawa hiyo marambili au tatu (huku ukiwa hujaingiza hewa)

  4. kisha achia hewa iingie ndani ya mapafu kwa kuvuta huku kikopo cha dawa kikiwa mdomoni

  5. kisha ondoa kikopo huku ukiwa umefunga mdomo na kaa kama sekunde 10-15 bila kutoa hewa nje ya mdomo wako.

  6. Baada ya hapo pumua kama kawaida

Kwa kufanya hivyo dawa itakuwa imeingia vizuri katika njia za mfumo wa hewa na kusababisha njia hizo kufunguka


Kumbuka; Dawa yenye mchanganyiko wa salbutamol(beta agonist) na corticosteroid huwa nzuri kwa sababu huweza kufanya mambo mawili ambayo hutokea kwenye asthma/pumu


Beta agonist- hufungua njia za hewa na kusababisha hewa ya ndani ya mapafu iingie na kutoka vema


Corticosteroid huzuia kuzalishwa kwa ute ute na kuvimba kwa njia za mfumo wa hewa.

kwa taarifa zaidi ingi katika link iliyo hapo juu



Kumbuka siku zote wasiliana na daktari wako kwa tiba na ushauri. Kupata ushauri kutoka kwa madaktari wetu piga simu kwa namba zilizo chini ya tovuti hii au wasiliana kwa email.

926 views0 comments

Recent Posts

See All

Comments


bottom of page