top of page

Maumivu katikati ya kifua| ULY CLINIC

Maumivu katika ya kifuaMaumivu katikati ya kifua mara nyingi hutokana na magonjwa ya ogani mbalimbali zilizo ndani ya kifua ya kifua na mara chache sababu zinaweza kuwa nje ya kifua au sehemu ya mbali na kifua. Mara nyingi husababishwa na magonjwa ya moyo, mapafu na ukuta wa dayaframu. Baadhi ya sababu zinahitaji matibabu ya haraka zaidi kwani mtu anaweza poteza uhai endapo hata pata msaada.


Endapo unapata maumivu yafuatayo unahitaji kupata msaada wa haraka.


 • Maumivu ya kifua yanayokuwa makali zaidi na kuhisi kama kifua kinachanika kwenye maeneo ya titi

 • Maumivu ya kifua yanayosambaa kwenye taya, mkono wa kushoto au mgongoni

 • Maumivu yanayoambatana na Kupoteza fahamu, mapigo ya moyo kwenda kasi na kupummua harakaharaka


Visababishi


Visababishi vya maumivu katikati ya kifua vinaweza kuwa;

 • Homa ya mapafu(nimonia)

 • Homa ya kifuko cha kongosho

 • Infaksheni ya mayokadiamu

 • Kolesistaitizi

 • Kubana kwa misuli ya kifua

 • Majeraha kwenye mbavu

 • Vidonda vya tumbo

 • Kucheua tindikali

 • Pumu ya kifua

 • Kostokondraitizi

 • Kusinyaa kwa mapafu

 • Magonjwa ya mijongeo ya misuli ya esofagasi

 • Kuchanika kwa mrija wa esofagasi

 • Henia ya hayatasi

 • Magonjwa ya mishipa ya moyo

 • Kuchanika kwa mshipa wa aotiki

 • Pankreataitizi

Bonyeza hapa kuendelea kusoma zaidi kuhusu makala hii


ULY Clinic inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchuku hatua yoyote ile inayohusu afya yako.

175 views0 comments

Recent Posts

See All

Comments


bottom of page