top of page

Maumivu ya chuchu/titi | ULY CLINIC

Updated: Aug 5, 2020



Maumivu ya matiti (mastalgia) ni dalili inayotokea mara kwa mara kwa wanawake, Dalili hii huweza kuwa, maumivu ya chuchu zikishikwa, maumivu ya kuchoma au kuunguza au kubana kwenye tishu zinazotengeneza matiti.

Maumivu hayo huweza kuwa makali au ya kawaida, na huweza kutokea

  • Siku chache za mwezi, siku mbili au tatu kabla ya kuanza hedhi yako ya mwezi. Kutokea kwa maumivu wakati huu ni kawaida, maumivu huwa kidogo au ya wastani na huweza husisha matiti yote mawili

  • Kwa wiki au Zaidi katika mwezi, huanza kabla ya kuona hedhi yako,na wakati mwingine huendelea katika kipindi chote cha hedhi. Maumivu huwa ya wastani au makali sana na huathiri matiti yote mawili

  • Maumivu yanayoedelea mwezi mzima au Zaidi, maumivu haya hayana mahusiano na mzunguko wa hedhi.

Wanawake wanaokaribia koma hedhi wakati mwingine hupata maumivu ya matiti, hata hivyo maumivu ya matiti hutokea sana kwa wanawake vijana ambao bado hawajafikia kwenye komahedhi


Mara nyingi maumivu ya chuchu huwa hayasababishwi na saratani na huwa haya maanishii una saratani. Licha ya hayo, maumivu ya matiti ambayo yanaendelea hata baada ya komahedhi au yasiyoisha baada ya mzunguko 1 au 2 ya hedhi huhitaji kufanyiwa uchuguzi wa ndani ili kujua visababishi.

dalili


Visababishi


wakati mwingine si rahisi kujua kisababishi cha maumivu ya matiti. Mambo yanayochangia kupata maumivu ya titi ni pamoja na;


Homoni za uzazi

Tafiti na ushahidi wa kisayansi huonesha maumivu ya chuchu huhusiana na mabadiliko ya kiwango cha homoni za uzazi zinazotofautiana katika mzunguko mzima wa hedhi. Maumivu ya titi ya kujirudia katika mwezi hupotea endapo mtu anatapa mimba au hedi itakoma


Umbo la titi

Maumivu ya titi yasiyohusiana na mzunguko wa hedhi hutokea kutokana na mabadiliko yanayotokea katika maumbile ya tezi mirija inayopitisha maziwa katika titi. Mabadiliko haya yanaweza kusababisha kutokea kwa vifuko vya maji kwenye chuchu. Kupigwa kwenye chuchu, kufanyiwa upasuaji au mambo mengine yanaweza kusababisha maumivu ya titi. Hata hivyo maumivu ya titi huweza kuanzia nje ya titi mfano kifuani, kwenye misuli, maungio ya mifupa na kisha kuelekea kwenye chuchu.


Kiwango cha faty aside

72 views0 comments

Recent Posts

See All

Comments


bottom of page