top of page

Mjamzito anapaswa kulalaje? | ULY CLINIC

Updated: Jun 29, 2020


Imeandikwa na madaktari wa uly clinic

Utangulizi

Kipindi cha ujauzito haswa pale mama anapoingia katika kipindi cha semister ya pili ama anapoanza miez mitatu ya ujauzito, mara nyingi huhisi uzito katika tumbo lake.


Binadamu wa kawaida kwenye tumbo lake kuna mishipa ya damu mikubwa iitwayo veins na atery ambayo pia hutumika kupeleka ama kutoa damu yenye virutubisho na hewa safi na uchafu kati ya mama na mtoto.


Uzito wa mtoto huweza kugandamiza mishipa hiyo na kusababisha kupungua  usafilisaji wa virutubisho na gesi safi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, na pia kuzuia usafilishaji wa gesi chafu na uchafu mwiingine kutoka kwa mtoto kwenda kwa mama kwa ajili ya kutolewa nnje ya mwili. Hivyo madhara ya mtoto kutokuwa vyema ama hata kupoteza maisha kwa mtoto kunaweza kutokea.


Ni upande gani mama anatakiwa kulalia?


Kwa kawaida mishipa mikubwa ya artey imepita upande wa kushoto wa tumbo, mishipa hii huwa na misuli hivyo hata ikigadamizwa huweza kudunda na kupitisha damu kirahisi(ni rahisi kuhimili uzito wa mtoto), Mishipa iliyopo kushoto mwa tumbo huwa haina misuli ya kutosha na hivyo endapo itagandamizwa na kitu kizito kama mtoto itaweza kuleta matatizo katika mzunguko wa damu wa mama na mtoto. Hivyo pozi sahihi la kulala kwa mama mjamzito ni kulalia ubavu wa kushoto


Imeboreshwa 29.06.2019


Soma zaidi kuhusu mazoezi sahihi kwa mjamzito kwa kubonyeza hapa


Usisahau kuwashirikisha watu uwapendao kupakua app ya ULY CLINIC

Karibu ULY CLINIC kwa tiba na ushauri.

102 views0 comments

Recent Posts

See All

Comments


bottom of page