top of page

Punguza uzito kwa maji ya moto|ULY CLINIC

Unywaji wa maji ya moto asubuhi kupunguza uzito


Ukweli kuhusu unywaji wa maji ya moto wakati kabla ya kula ili kupunguza uzito

Maji ni kimiminika muhimu sana katika uso wa dunia na maisha ya binadamu, tafiti zinaonyesha kuwa uso wa dunia umetengenezwa kwa maji kwa asilimia 71, na hivyo hivyo uzito wa binadamu unatokana na maji kwa asilimia zaidi ya 60 wakati huo nyama, mifupa na mafuta vimechangia asilimia 40 tu ya uzito wa binadamu.Uwepo wa maji mengi duniani unadhihirisha umuhimu wake katika mfumo wa ekolojia. Inashauriwa na wataalamu wa afya kutumia glasi nane za maji kwa siku, hii ikiwa inamaanisha lita mbili za maji kwa siku endapo huna tatizo lolote linalokufanya usitumie maji.


Ifahamike kwamba mahitaji ya maji mwilini hutegemea shughuli anazofanya mtu, mfano mtu anayelima juani na anayefanya mazoezi hupoteza kiwango kikubwa cha maji kupitia ngozi, pumzi n.k hivyo mahitaji ya maji yataongezeka zaidi ya lita mbili ukilinganisha na mtu mwenye maisha ya kukaa au kutofanya shughuli za kumtoa jasho.

Makala hii imejikita kuangalia umuhimu wa maji ya moto katika mwili wa binadamu, kubwa likiwa ni usemi unaofahamika kuwa unywaji wa maji ya moto asubuhi husaidia kupunguza uzito


Je maji ya moto yanapunguzaje uzito?


Kunywa maji ya moto huleta hisia za shibe, hali hii inaweza kukufanya ule chakula kidogo na kufanya mwili upate nguvu kiasi kidogo tu na hivyo kusababisha usiongezeke uzito. Hata hivyo kunywa maji ya moto husaidia kuongeza ufyonzwaji wa chakula na kuondoa sumu mwilini.


Tafiti ya kuangalia mchango wa maji ya moto katika kuongeza uzalishaji joto mwilini ilionyesha kwamba, kunywa maji ya moto kiasi cha mililita 500 huongeza uzalishaji joto mwilini na hivyo mwili hutumia nishati ya kilojoules 100. Hii inamaanisha kwamba matumizi ya maji ya moto lita mbili kwa siku yatafanya mwili utumie kilojoules 400.

Kwa kawaida binadamu anahitaki kiasi cha kilojoules 8368 (2000kCal) kwa siku kwa mwanamke na 10460 (2500kCal) kwa siku kwa mwanaume


Hivyo utumiaji wa maji ya moto kila siku husaidia mwili wa binadamu kuongeza matumizi ya nishati mwilini zilizohifadhiwa kama wanga au mafuta na hivyo kupelekeakupunguza uzito na kuongeza hisia za kushiba.


Jumuisho, kupungua kwa uzito kutokana na kunywa maji ya moto asubuhi au kabla ya kula chakula hukufanya upungue uzito kwa njia hizi tatu

 1. Kuongeza umetaboli mwilini

 2. Kuongeza uvunjwaji wa mafuta mwilini

 3. Kukata/kupunguza njaa

Faida zingine za maji ya moto ni

 • Kuondoa tatizo la kupata haja ngumu

 • Kutuliza mfumo wa fahamu, hivyo kukufanya usihisi maumivu makali na kutokuwa na msongo mwilini kwa kuongeza mzunguko wa damu huongezeka mwilini

 • Kuondoa sumu mwilini kupitia jasho

 • Kuongeza umeng’enyaji wa chakula tumboni

 • Kuzibua njia za hewa kwa wale wenye mafua kutokana na virusi au kuziba kwa sainas


Ushauri kuhusu matumizi ya maji ya moto

 • Usitumie maji ya moto zaidi ya nyuzi joto 70C ili kuepuka kuungua na kupata vidonda mdomoni

 • Kwa matokeo mazuri ya kupunguza uzito tumia maji ya moto mililita 500, sawa na nusu lita nusu saa kabla ya kula au baada ya kula. Unaweza kuweka viungo kwenye maji hayo ili kukula ladha zaidi au kutumia bila kiungo chochote.

 • Kwa wagonjwa mfano wagonjwa wa moyo na figo hakikisha unafuata ushauri wa daktari wako kuhusu kiwango cha maji unachotakiwa kutumia kwa siku.

Soma zaidi kuhusu umuhimu wa maji mwilini na mambo yanayoongeza matumizi ya maji kwa kubonyeza kpengele unachopenda.

 1. USGS.How Much Water is There on Earth? - USGS.https://www.usgs.gov/special-topic/water-science-school/science/how-much-water-there-earth?qt-science_center_objects. Imechukuliwa 12.11.2020

 2. USGS.The Water in You: Water and the Human Body. https://www.usgs.gov/special-topic/water-science-school/science/water-you-water-and-human-body . Imechukuliwa 12.11.2020

 3. E. times. Weight loss: Does sipping on hot water really help you lose belly fat?. https://timesofindia.indiatimes.com/life-style/health-fitness/weight-loss/weight-loss-does-sipping-on-hot-water-really-help-you-lose-belly-fat/photostory/77286556.cms# . Imechukuliwa 12.11.2020

 4. Pubmed. Water-induced thermogenesis. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/14671205/ . Imechukuliwa 12.11.2020

 5. Medical news today. What are the benefits of drinking hot water?. https://www.medicalnewstoday.com/articles/319673 . Imechukuliwa 12.11.2020

 6. Lumen. Chemistry for non-majors. Thermochemistry. https://courses.lumenlearning.com/cheminter/chapter/energy-in-food-and-nutrition/. Imechukuliwa 12.11.2020

 7. NHS.UK.What should my daily intake of calories be?.https://www.nhs.uk/common-health-questions/food-and-diet/what-should-my-daily-intake-of-calories-be/#. Imechukuliwa 12.11.2020

454 views0 comments

Recent Posts

See All

Comments


bottom of page