top of page

Tatizo la ngozi kuwa na michirizi na weusi-Acanthosis nigricans


Acanthosis nigricans ni hali ya ngozi inayoonekana kwa ngozi kuwa na michirizi au miinuko mweusi yenye unyevu katika maeneo kadhaa ya mwili, ngozi iliyoathirika inaweza kunenepa. Mara nyingi, acanthosis nigricans huathiri kwapa, kinena na shingo.

Mabadiliko ya ngozi ya acanthosis nigricans (ak-an-THOE-sis NIE-grih-kuns) hutokea kwa watu ambao wana uzito kupita kiasi (BMI zaidi ya 25) au wana ugonjwa wa kisukari. Watoto wanaopata halii hii wana hatari kubwa ya kupata kisukari cha aina 2 wakiwa wakubwa. Mara chache, acanthosis inaweza kuwa ishara ya saratani katika ogani zilizo ndani ya mwili, kama vile tumboni au kwenye ini.

Hakuna tiba maalum inayopatikana kwa tatizo hili la acanthosis. Matibabu huelekezwa kwenye kisababishi.Matibabu ya kisababishi huweza kurejesha umbile na rangi ya kawaida yangozi kwa kutibu

Dalili

Mabadiliko ya ngozi ni ishara pekee za acanthosis nigricans. Utaona ngozi yenye giza, yenye unyevu, yenye miinuko au michirizi katika mikunjo ya mwili- kwa kawaida kwenye kwapa,kinena na nyuma ya shingo. Mabadiliko ya ngozi kawaida huonekana polepole. Ngozi iliyoathiriwa inaweza pia kuwa na harufu au kuwasha.

Visababishi

Upinzani dhidi ya Insulin

Watu wengi wenye tatizo hili huwa pia na upinzani kwenye homoni ya insulin. Insulin ni homoni inayozalishwa na tezi kongosho, husaidia mwili utumie sukari. Upinzani dhidi ya insulin huweza sababisha kisukari aina ya 2


Matatizo ya homoni

Tatizo la acanthosis mara nyingi hutokea kwa watu wenye matatizoya kihomoni kama kuwa na vifuko vya maji kwenye ovam. Upungufu wa homoni ya thyroid, na Matatizo katika tezi inayozalisha adrenalini.


Matumizi ya dawa aina fulani

Dozi kubwa ya vitamin B3 (Niacin), dawa za uzazi wa mpango, dawa ya prednisone, na dawa zingine jamii ya corticosteroid huweza sababisha tatizo la acathosis.


Saratani

Saratani aina kadhaa zinaweza kuambatana na saratani kama, saratani yalymphoma, saratani ya tumbo,utumbo mpana na saratani ya ini.


Vihatarishi

  • Uzito kupita kiasi

  • Jinsi uzito unavyoongezeka unapata kihatarishi cha kupata tatizo hili

  • Historia Tatizo hili kwenye familia

  • Kuwa mtu wa mataifa ya afrika

Vipimo

Maranyingi tatizo huonekanawakati wa uchunguzi wa mwili, endapo kisababishi hakitafaamika kutoka kwenye historia ya mgonjwa basi daktari anaweza agiza baadhi ya vipimo vya damu na X ray ili kuangalia kisababishi

Madhara

Watu wenye tatizo la acanthosis huweza kuelekea kupata kisukari aina ya 2

Matibabu

Matibabu huhusisha kutibu kisababishi

  • Mfano kupunguza uzito endapo tatizo limesababishwa na uzito kupita kiasi

  • Kuacha/ kusimama kunywa dawa aina Fulani inayoleta tatizo hilo

  • Kufanyiwa upasuaji wa kurekebisha ngozi


Toleo la 1

Imechapishwa 12/11/2018

66 views0 comments

Recent Posts

See All
bottom of page