top of page

Tumia simu yako ya mkononi kupata majibu elimu na huduma za ki Afya kutoka kwa ma Daktari Tanzania

Updated: Feb 21, 2020Kwa sasa ikiwa wewe ni mtanzania na unamaswali mengi unayo jiuliza kuhusu Afya yako au umepata mabadiliko yoyote ya mwili na huelewi ni nini, huna haja ya kuhofu kwani unaweza kupata huduma za kuuliza na kupata majibu kutoka kwa madaktari wazoefu kwenye mambo ya elimu, ushauri na Tiba waliosajiliwa na baraza la madaktari Tanzania


Imekuwa mtu akienda Hospitali hapati maelezo ya kutosha kuhusu dawa au vipimo ambavyo atafanyiwa au anafanyiwa, hivyo imeleta wasiwasi kwa mgonjwa kuhusu anachofanyiwa kina faida au la. MAdaktari wetu wapo kujibu maswali yoyote yale ambayo unajiuliza kuhusu hali yako ya mwili, dawa, dalili zozote zile unazoumwa na kupata majibu na pengine ushauri endapo utahitaji kuhusu vipimo gani ufanye, dawa gani utumie na ushauri mwingine.


Kumbuka taarifa zako ni siri ya wewe na daktari, usiri huo unazingatiwa kwa kila mgonjwa au mtumiaji wa mtandao huu.


Kurahisisha huduma na kusoma makala za ki Afya kwenye tovuti yetu ni vema ukapakua au "Install application" yetu ya uly clinic kwa kubonyeza kiunganishi au link hii hapa

85 views0 comments

Recent Posts

See All

Kommentare


bottom of page