Shinikizo la juu la damu kama lisipopata matibabu huleta madhara makubwa mwilini kama vile kiharusi na moyo kufeli. Miongoni mwa mambo ya msingi katika matibabu ni elimu kwa mgonjwa.
Kuna mahusiano makubwa ya shinikizo la juu la damu na chakula. Mtu mwenye dalili za kwanza za shinikizo au mwenye shinikizo anashauriwa kubadili mfumo wa maisha yake ili kudhibiti shinikizo hili.
Visababishi vya shinikizo la damu la juu linalohitaji matibabu
Shinikizo la damu huongezeka kwa haraka kama mgonjwa ameacha kutumia dawa na hivyo kuweza kusababisha kuhitaji matibabu ya haraka. Tumia dawa ipasavyo na kufuata ushauri wa daktari ili kudhibiti shinikizo la damu.