top of page
Tafiti za Afya Mtandaoni
Karibu kwenye ulimwengu wa utafiti
Tafiti za Afya Mtandaoni
Karibu kwenye ulimwengu wa utafiti

Tafiti na Ufadhiri wa tafiti 

Katika ulimwengu wa mtandao watu wengi wangependa kukusanya taarifa za haraka na kutoka kwa watu walio maeneo mbalimbali. Mtandao wetu una watumiaji wengi wa huduma za afya.  Kupitia mtandao wetu unaweza kufanya tafiti mbalimbali zikilenga kutambua visababishi, vihatarishi na elimu kuhusu mambo mbalimbali ya  afya

Changia katika kuleta matokeo chanya kwenye huduma za afya na tiba Afrika kwa kufanya tafiti ambazo zinaleta mabadiliko kwenye jamii.

Ufadhiri wa kufanya Tafiti

ULY clinic kupitia mfuko maalumu wa Tafiti, inafadhiri tafiti mbalimbali zinazolenga kusaidia jamii kwenye mambo ya afya. Tunakaribisha maombi ya ufadhiri wa kufanya tafiti kutoka kwa wadau mbalimbali wa afya ndani na nje ya nchi (Nchi zilizo Afrika).

 

Ufadhiri unaotolewa ni wa aina mbalimbali, na unaweza kuhusisha shughuli zote au baadhi tu.

 

Mara baada ya kutuma maombi yako Watafiti wa ULY CLINIC watapitia maombi yako ya ufadhiri kisha utapewa utaratibu wa kupata ufadhili.

Tunakaribisha wazalendo wote wanaoipenda Afrika na wanaotamani kutokea kwa mabadiliko makubwa kwenye tiba, kuanzia matumizi ya tekinolojia n.k 

Jihusishe kutoa taarifa kwenye tafiti zinazoendelea kwa kubonyeza aina ya tafiti zilizo kwenye kuraha hii

Ni zamu yako sasa kuboresha huduma za afya kwa kuchangia taarifa tu!

 

Sisi tunatimiza kwa kukupa maarifa ya Afya kupitia tovuti hii


Jaza fomu kuchangia taarifa sasa
 
Kwa kujaza fomu moja tu utachangia  kuleta mabadiliko katika huduma za afya Afrika.
 
Bofya kitufe kujaza fomu zilizoorodheshwa hapa chini ili kuchangia taarifa muhimu zitakazosaidia kuboresha utoaji wa huduma za afya Afrika. Kumbuka kumaliza kujaza maelezo kwenye fomu tafadhali.

 
KUMBUKA- Taarifa zako ni siri na zitatumiwa kuboresha huduma za afya. Changia mara moja tu kwa tafiti aina moja, endapo pia sio muhisika katika tafiti, usichangie. Mfano tafiti za kina mama wajawazito zinatakiwa kujazwa na wamama wajawazito tu.

Tafiti za kisukari
Tafiti za kifafa

Tafiti muhimu zinazohitaji taarifa zako

bottom of page