top of page
Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD,
Mhariri:
Dkt. James NL, MD
Imeboreshwa:
16 Oktoba 2026, 07:20:56

Je, ikiwa mtoto amejizonga na kitovu shingoni, mama anaweza kujifungua kwa njia ya kawaida?
Mama anaweza kujifungua kwa njia ya kawaida hata kama mtoto amejizungusha kitovu shingoni. Hali hii pekee si sababu ya lazima ya kufanyiwa upasuaji.
- Ufuatiliaji: Ni muhimu kufuatilia mapigo ya moyo wa mtoto na maendeleo ya uchungu ili kubaini mapema dalili za mtoto kupata shida.
- Dalili zinazoweza kuhitaji upasuaji: Mapigo ya moyo wa mtoto kushuka au kubaki katika hali isiyo ya kawaida, dalili za mtoto kukosa oksijeni, au uchungu kutokuendelea licha ya usimamizi unaofaa. Uamuzi hutegemea tathmini ya haraka ya timu ya uzazi.
- Muhimu: Uamuzi wa njia ya kujifungua hutegemea hali ya mama na mtoto, si kitovu kuzunguka shingo pekee.
Soma zaidi kuhusu mtoto kujizungushia kitovu shingoni kwa kubofya 👉 Mtoto kujifunga na kitovu wakati wa ujauzito
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeandikwa,
15 Oktoba 2026, 16:36:26
bottom of page

