top of page

Mwandishi:

Dkt. Benjamin L, MD

Mhariri:

Dkt. Rachel L, MD

Ijumaa, 30 Juni 2023

Ke, unaongezaje hisia zako za ngono?

Ke, unaongezaje hisia zako za ngono?

Mwanamke anawezaje kuongeza hisia zake za ngono?


Ikiwa wewe ni mwanamke na umekuwa ukikosa hamu ya ngono, unaweza kujiuliza ni njia gani unaweza kutumia ili kuongeza hamu na hisia za kingono. Makala hii fupi inaweza kukusaidia kufahamu baadhi ya njia. Kwa maelezo zaidi unaweza kufuatilia makala zinazoongezwa katika tovuti hii au kuwasiliana na daktari kupata maelezo zaidi kwenye kila njia.


Hamu ya ngono ni nini?

Hamu ya ngono ni hali ya kuwa na hisia, msukumo na hamasa ya kujihusisha na shughuli za kingono ambazo hutokana na msukumo wa ndani au nje ya mwili.


Matibabu takatifu ya kutokuwa na hamu ya ngono huhusisha tiba mwili, homoni, saikolojia na hisia. Mfano mtu hawezi kuwa na hamu ya ngono kama ana hisia hasi au ana ugonjwa unaovuruga homoni mwilini mwake. Kidokezo hiki kimezungumzia kuhusu njia anazoweza kutumia mwanamke kuongeza hamu ya ngono.



Njia za kuongeza hamu ya ngono kwa mwanamke

Njia zinazoongeza hamu na hisia za ngono ni pamoja na Kufanya mazoezi, kuacha msongo, kuongea na mwenza, kuweka kwenye ratiba tendo la ngono, kuongeza manjonjo kwenye ngono na kuacha tabia hatarishi. Maelezo ni kama yalivyo hapa chini.


Fanya mazoezi

Kufanya mazoezi ya kiaerobiki na ya kuimarisha mwili mbali na kuongeza uimara wa mwili na mwonekano, huongeza hisia za mwili kwenye ngono. Mazoezi yoyote yanayofanya mwili utoke jasho ikiwa pamoja na kazi za bustani au shamba yanaweza kufanyika. Kufanya mazoezi hurekebisha homoni mwilini kwa kuleta homoni za tulizo na hamu ya ngono baada ya mazoezi. Mazoezi yanapaswa kuambatana na kula mlo kamili na unaoshauriwa kuongeza hisia za kingono.

  

Epuka msongo

Msongo wa mwili ni njia nyingine inayopelekea mvurugiko wa homoni za utulivu na ngono mwilini na hupelekea mwili kuchoka haraka na mtu kutofurahia maisha. Zipo njia njema za kuepuka msongo unazoweza kutumia kwa hatima njema ya maisha yako. TTumia njia hizo kukabiliana na msongo mwilini kutokana na kazi, pesa na mahangaiko ya kila siku ya kimaisha ili hatimaye ipelekee ongezeko la hamu ya ngono.


Ongea na mwenza

Kufanya mazungumzo na mwenza na kuambiana ukweli na kwa uaminifu kuhusu mambo unayopenda na usiyopenda huleta muungano imara na hisia kuu kwa mwenza na kwenye tendo la ngono.


Kuwa na ratiba ya kufanya ngono

Mwili huwa na kumbukumbu kama utakuwa na ratiba ya kujirudia mara kwa mara. Ni kama mtu akiwa na ratiba ya kula mua ule ule kila siku, vimeng'enya na homoni huzalishwa kwa wingi muda mfupi kabla ya muda wake wa kula, hii hufanyika hata kama hakuna chakula wala harufu yake kwa sababu mwili unakuwa umeshaweka kumbukumbu ya muda. Kuwa na ratiba maalumu ya ngono kila baada ya siku chache au kila siku fulani katika wiki, mbali na kufanya mwili ujitengenezee utaratibu wa kukukumbusha kupitia homoni za ngono n.k hufanya ufurahie ngono na kuridhika. Licha ya kupanga muda wa ngono katika ratiba yako inaweza kuwa jambo lisilo na umuhimu na kuboa, kulipangia muda katika ratiba yako kutafanya urejee upya kuwa na hisia thabiti za kingono.


Ongeza manjonjo wakati wa kufanya ngono

Manjonjo kiasi kwenye ngono huwa kama kiungo katika chakula, humfanya mtu kupata radha mpya na ongezeko la hamu ya ngono.


Manjonjo yanaweza kufanywa kwa kubadilisha pozi tofauti la ngono badala ya lile ulilozoea au kubadilisha mazingira ya kufanyia ngono kwa kwenda sehemu nyingine mbali na unapoishi au chumba kingine ndani ya sehemu unayoishi.


Muombe mpenzi wako kutumia muda mwingi kukusisimua hisia zaidi ya muda unaotumia katika kufanya tendo lenyewe. Unaweza kutumia vifaa saidizi vya kusisimua mwili pia kama mnamaelewana ya kutumia vifaa hivyo na mwenza wako.


Acha tabia hatarishi

Kutumia sigara, madawa ya kulevya na matumizi ya pombe ya kupindukia yanaweza kupunguza hisia za kingono. Kuachana na tabia hizi kutafanya afya yako kurejea kama awali na kupata hisia zaidi za ngono.


Vyakula vya kuongeza hisia za ngono

Hisia za ngono mbali na kuongozwa na akili, huongozwa pia kwa sehemu kubwa na homoni mwilini. Kuongeza hisia za kingono ongeza vyakula vinavyoongeza hamasa ya kingono katika mlo wako. Vyakula hivyo vimezungumziwa maeneo mengine katika tovuti hii.


Pata usingizi wa kutosha

Weka muda wa kutosha kulala, kama ukiwa na hisia za uchovu wa mwili hutawaza kuhusu ngono. Kutopata usingizi wa kutosha huwa na athari hasi kwenye kila kitu kuanzia mahusiano yako na kwenye homoni za kijinsi. Inashauriwa kulala kwa angalau masaa 8 wakati wa usiku.


Kutumia virutubisho na dawa asili

Dawa asili ambazo zimetengeneza kutoka kwenye mimea zinaweza kutumika katika matibabu ya kukosa hamu ya ngono. Matumizi ya dawa za hospitali za kuongeza hamu ya ngono ni uchaguzi wa mwisho kutokana na madhara yake mwilini.


Makala zingine zinazohusu ngono

Kusoma kuhusu makala zingine zinazohusu vyakula na ngono, usingizi na mazoezi bofya linki zinazofuata:


ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

2 Agosti 2024 18:41:45

Rejea za mada hii:

1. Shifren JL. Sexual dysfunction in women: Epidemiology, risk factors, and evaluation. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 30.06.2023

2. Longo DL, et al., eds. Sexual dysfunction. In: Harrison's Principles of Internal Medicine. 19th ed. New York, N.Y.: The McGraw-Hill Education; 2015. http://accessmedicine.mhmedical.com. Imechukuliwa 30.06.2023

3. Hoffman BL, et al. Psychosocial issues and female sexuality. In: Williams Gynecology. 3rd ed. New York, N.Y.: McGraw-Hill Education; 2016. http://accessmedicine.mhmedical.com. Imechukuliwa 30.06.2023

4. Lodise NM. Female sexual dysfunction: A focus on flibanserin. International Journal of Women's Health. 2017;9:757.

5. Shifren JL. Overview of sexual dysfunction in women: Management. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 30.06.2023

6. Goldstein I, et al. Hypoactive sexual desire disorder: International Society for the Study of Women's Sexual Health (ISSWSH) expert consensus panel review. Mayo Clinic Proceedings. 2017;92:114.

7. Hirsch M, et al. Sexual dysfunction caused by selective serotonin reuptake inhibitors (SSRIs): Management Sexual dysfunction caused by selective serotonin reuptake inhibitors (SSRIs):

8. ManagementSexual dysfunction caused by selective serotonin reuptake inhibitors (SSRIs): Management. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 30.06.2023

bottom of page