top of page

Mwandishi:

Dkt. Lusenge S, MD

Mhariri:

Dkt. Sospeter M, MD

Jumamosi, 8 Julai 2023

Njia nzuri ya kuongeza damu

Njia nzuri ya kuongeza damu

Upungufu wa damu hutokea pale ambapo kiwango cha chembe nyekundu za damu au kiwango cha himoglobini katika chembe nyekundu za damu kinapokuwa chini ya kiwango cha kawaida. Zipo sababu nyingi zinazopelekea upungufu wa damu, sababu inayoongoza sana ni upungufu wa virutubisho kama madini chuma na vitamini.


Ni njia ipi nzuri ya kuongeza damu?

Njia ya kuongeza damu hutegemea kiwango cha upungufu wa damu, yaani kiwango kidogo hadi kiwango kikubwa sana kinacho hatarisha maisha. Viwango hivi vya upungufu wa damu hutafsiriwa kwa kupima kiwango cha himoglobini katika chembe nyekundu za damu. Kwa ujumla kuna njia kuu tatu za kuongeza kiwango cha damu ambazo zimeorodheshwa hapa chini.


Dawa za kuongeza damu

Dawa kama vile FEFO, Ferrous sulphate na Folic acid hutumika. Njia hii ni nzuri kwa mgonjwa mwenye kiwango kidogo na cha kati cha upungufu wa damu. Maelezo zaidi yanapatikana kwenye makala ya dawa za kuongeza damu.


Tiba lishe

Ni njia nzuri kwa mgojwa mwenye kiwango kidogo na cha kati cha upungufu wa damu. Huhusisha kula mlo kamili wenye madini chuma, vitamin B na C. Baadhi ya vyakula hivyo ni;

  • Nyama

  • Mayai

  • Maharagwe

  • Samaki na viumbe wengine wa kwenye maji

  • Mboga za majani za kijani

  • Mbegu

  • Karanga


Kuongezwa damu

Ni njia nzuri kwa mgonjwa mwenye kiwango kikubwa sana cha upungufu wa damu kinacho hatarisha maisha.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

2 Agosti 2024 18:30:16

Rejea za mada hii:

1.Anaemia – World Health Organization (WHO). https://www.who.int/health-topics/anaemia#tab=tab_1. Imechukuliwa 04.07.2023

2.Iron-Rich Food | List of Meats And Vegetables - Red Cross blood donation.redcrossblood.org. https://www.redcrossblood.org/donate-blood/blood-donation-process/before-during-after/iron-blood-donation/iron-rich-foods.html. Imechukuliwa 04.07.2023

3.15 Healthy Foods That Are High in Folate (Folic Acid) – Healthline.com.https://www.healthline.com/nutrition/foods-high-in-folate-folic-acid. Imechukuliwa 04.07.2023

4.FEFOL SPANSULE CAPSULES.Drugs.com. https://www.drugs.com/uk/fefol-spansule-capsules-leaflet.html#. Imechukuliwa 04.07.2023

bottom of page