top of page

Vidokezo vya Afya

Kupasuka kwa chupa ya uzazi kabla ya uchungu

Kupasuka kwa chupa ya uzazi kabla ya uchungu

Kupasuka kwa chupa ya uzazi kabla ya uchungu ni kuchanika kwa kuta za chupa ya uzazi kabla uchungu kuanzana baada ya ujauzito kutimiza wiki 37, hali hii ni kawaida kutokea kwenye ujauzito 10 kati ya 100.

Kupata ujauzito baada ya kutoa mimba

Kupata ujauzito baada ya kutoa mimba

Unaweza kupata ujauzito ndani ya siku 14 baada ya kutoa mimba, hata hivyo kama una mzunguko mfupi wa hedhi unaweza kupata mapema zaidi. Unashauriwa kutumia kondomu ili kuzuia mimba isiyotarajiwa.

Kupunguza uzito, kunywa maji kabla ya kula

Kupunguza uzito, kunywa maji kabla ya kula

Kunywa nusu lita ya maji ya uvuguvugu dakika 30 kabla ya mlo wowote ule, ikifuatiwa na kula chakula chenye nishati kidogo. Tabia hii huchangia kwa kiasi kikubwa kupunguza uzito mkubwa kupita kiasi.

Kushindwa kunyonya, homa, mwili kulegea

Kushindwa kunyonya, homa, mwili kulegea

Kushindwa kunyonya, homa, mwili kulegea ni dalili za magonjwa kwa mtoto mchanga, mwahishe hospitali kwa tiba sahihi.

Kushusha homa kwa vichanga na watu wazima

Kushusha homa kwa vichanga na watu wazima

Mtoto chini ya umri wa miezi mitatu, endapo ana joto la mwili nyuzi za selisias 38 au zaidi, wasiliana na daktari wako mara moja kwa ushauri na tiba. Kwa watoto zaidi ya umri wa miezi mitatu na watu wazima, pumzisha mwili, kunywa maji ya kutosha. Tumia panadol au ibuprofen kutuliza homa endapo kuna ulazima, na endapo homa imedumu zaidi ya siku tatu onana na daktari wako mara moja.

bottom of page