top of page

Vidokezo vya Afya

Chai ya rozela

Chai ya rozela

Kunywa vikombe vitatu vya chai ya rozela hudhibiti mapigo ya moyo, hupunguza lehemu na mafuta yaliyoshamiri kwenye damu. Kwa kufanya hivyo hulinda mishipa ya damu na kudhibiti kwa kiasi kikubwa shinikizo la juu la damu.

Chanjo za UVIKO-19

Chanjo za UVIKO-19

Mwili una uwezo asili wa kutengeneza kinga dhidi ya vimelea wa maradhi inayomlinda mtu baada ya maambukizi ya awali. Kwa kuwa kinga asili dhidi ya kirusi cha COVID-19 hudumu kwa muda mfupi, unashauriwa kupata chanjo ili kuuwezesha mwili wako kutengeneza kinga ya muda mrefu itakayokuepusha na ugonjwa mkali.

Chumvi na presha ya kupanda

Chumvi na presha ya kupanda

Matumizi ya muda mrefu ya chakula chenye chumvi nyingi husababisha ugonjwa wa presha ya kupanda. Watu zaidi ya milioni 7 hufa kwa ugonjwa huu kila mwaka duniani, walionusurika kifo hupata kiharusi na magonjwa mbalimbali ya moyo. Usiache kutumia chumvi, tumia kwa kiwango kinachoshauriwa kiafya.

Dalili za hatari kwa kichanga

Dalili za hatari kwa kichanga

Dalili za hatari wa Mtoto hutumika kuonyesha Mtoto yupi anatakiwa kupelekwa hospitali mapema iwezekanavyo anapokuwa na dalili hizo kwa ajiri ya matibabu.

Dalili zinazoambatana na kuota meno

Dalili zinazoambatana na kuota meno

Homa, kukuna masikio, kuhara, kukosa hamu ya kula na harara usoni ni baadhi ya dalili zinzohusishwa na kuota meno ya kwanza kwa watoto. Tafiti kadhaa zinaonyesha kuwa kuna uhusiano hafifu uliopo.

bottom of page