top of page

Vidokezo vya Afya

Syndrome ya Asherman

Syndrome ya Asherman

Asilimia 30 ya wanawake wanaokwanguliwa kizazi ili kutoa mimba yenye miezi mitatu au zaidi, hupata makovu makali ndani ya kizazi yanayosababisha ‘Syndrome ya Asherman’. Watu wenye syndrome hii hupata matatizo ya uzazi kama maumivu makali ya hedhi, kutokuona hedhi, ugumba n.k. Tumia njia za uzazi wa mpango, epuka kupata au kutoa mimba zisizotarajiwa.

Tabia ya kukufanya upate usingizi kwa wakati

Tabia ya kukufanya upate usingizi kwa wakati

Lala na amka muda uleule kila siku, zima taa kutengeneza giza na hakikisha hakuna kelele yoyote, zima na weka simu mbali na kitanda, usile mlo mkubwa wala kunywa kahawa au pombe masaa matatu kabla ya kulala na fanya mazoezi au kazi ya kukutoa jasho wakati wa mchana.

Tangawizi kwa mjamzito

Tangawizi kwa mjamzito

Chai ya tangaziwi inayopunguza kichefuchefu na kutapika wakati wa ujauzito, haipaswi kutumika katika kipindi cha mwisho na wakati wa uchungu ili kuepusha hatari ya kutokwa damu nyingi wakati wa kujifungua.

Tiba takatifu ya kiharusi mpito

Tiba takatifu ya kiharusi mpito

Tiba ya dawa na kinga inayotolewa kwa usahihi na wataalamu wa afya endapo ikihusisha athari zinazotokana na kiharusi mpito hufanya matibabu ya mgonjwa kuwa takatifu.

Tovuti salama kwa ushauri wa afya

Tovuti salama kwa ushauri wa afya

Kuna zadi ya tovuti 70,000 za afya duniani zinaongezekaa kila kukicha, ni jukumu la mtumiaji kufahamu namna ya kutambua na kutumia vyanzo salama ili kuepuka madhara. Baadhi ya sifa ya chanzo salama ni kuonyesha madhumuni ya tovuti, mada zimeandikwa na kuhaririwa na mtaalamu wa afya na kutoshawishi mtumiaji kununua au kutafuta huduma kutoka kwenye chanzo tu.

bottom of page