Vidokezo vya Afya

Usitupe chooni au kuchimbia aridhini dawa zilizoisha muda wa matumizi
Dawa zilizokwisha muda wake hupaswa kuteketezwa kwa utaratibu maalumu. Endapo umepewa maelekezo ya namna ya kuteketeza dawa zisizotumika, fuata maelekezo hayo kuziteketeza.Endapo hujapewa, zirejeshe kwa mfamasi au hospitali ili zikateketezwe kwa usalama. Usitupe chooni au kuchimbia aridhini, kuepuka madhara ya kiafya.

Usugu wa vimelea vya maradhi kwenye dawa
Matumizi yasiyo sahihi ya dawa jamii ya ‘antibiotic’ na ‘antifungal’ zinazotibu magonjwa mbalimbali kama kisonono, TB, UTI, tonses, nimonia, homa ya matumbo, fangasi ukeni n.k, husababisha vimelea kuwa sugu na kutotibika na dawa hizo. Tumia dawa kama ulivyoandikiwa na daktari wako.

Utambuzi wa jinsia ya mtoto tumboni
Wajawazito wanaweza kutambua jinsia ya mtoto kupitia DNA-PCR, ultrasound, au CVS, kila moja ikiwa na umri unaopendekezwa na kiwango cha usahihi tofauti. Kufahamu jinsia kunasaidia kupanga maandalizi, kupunguza msongo, na kuimarisha uhusiano wa mama na mtoto tumboni.


