top of page

Vidokezo vya Afya

Ivermectin imethibitishwa kutibu COVID-19

Ivermectin imethibitishwa kutibu COVID-19

Ivermectin, inayotumika kutibu maradhi ya vilemea mbalimbali, imeonekana katika tafiti kuwa na uwezo wa kuzuia usafirishaji wa protini muhimu zinazotengeneza kirusi, kuzuia kujishikiza kwa kirusi kwenye ukuta wa seli ya binadamu na kuzuia uzalishaji wa kemikali zinazoleta dalili kali za COVID-19.

Jali afya yako, fanya ngono salama

Jali afya yako, fanya ngono salama

Kufanya ngono salama itakulinda dhidi ya mimba zisizotarajiwa na maradhi ya VVU, kaswende, kisonono n.k. Ili ufanye ngono salama, fahamu na tumia kinga zilizopo, mfano PrEP itakukinga kupata VVU, kondomu itakukinga kupata mimba, magonjwa ya zinaa ikiwa pamoja na VVU. Jali afya yako kwanza.

Jiepushe na magonjwa kwa kula vema

Jiepushe na magonjwa kwa kula vema

Chakula bora ni mlo kamili unaoshauriwa kiafya, mtu mzima anapaswa kula angalau gramu 400 za mchanganyiko wa matunda mbalimbali na mboga za majani kila siku. Fanya hivi ili ujiepushe na magonjwa mengi kama kisukari, magonjwa ya moyo, kiharusi na saratani.

Jifunze tabia tano za kiafya

Jifunze tabia tano za kiafya

Pata kifungua kinywa cha kiafya, kula matunda na mboga za majani angalau mara tatu kwa siku, kula chakula kutoka kwenye nafaka zisizokobolewa, tumia chakula kilichopikwa kwa mafuta ya kiafya na fanya mazoezi angalau dakika 30 kila siku. Tabia hizi zitaufanya mwili wako uwe imara na afya njema.

Jikinge na maradhi ya tumbo, tumia maji safi

Jikinge na maradhi ya tumbo, tumia maji safi

Kwa kutumia maji safi na salama, utajikinga na magonjwa ya tumbo zaidi ya 20, ikiwa pamoja na homa ya taifodi, kipindupindi, giardiasis, dysentery, salmonellosis, Hepatitis A n.k. Kunywa, piga mswaki, safisha matunda na mboga za majani kwa maji safi yaliyotiwa chlorine au kuchemshwa, kula chakula kilichoiva vema na kutoa mvuke.

bottom of page