top of page

Vidokezo vya Afya

Karanga ya Lozi huondoa wasiwasi na kuleta usingizi

Karanga ya Lozi huondoa wasiwasi na kuleta usingizi

Tumia gramu 28 sawa na karanga 12 za lozi kila siku ili kupunguza na kutibu tatizo la kukosa usingizi na wasiwasi uliopitiliza. Karanga hii huongeza kiwango cha hormoni serotonin, homoni inayokufanya uwe mtulivu na ulale usingizi mwororo.

Kaswende kwa mtoto akiwa tumboni

Kaswende kwa mtoto akiwa tumboni

Magonjwa ya mama katika ujauzito kama kaswende huweza kumpata mtoto akiwa tumboni. Pima afya yako unapopanga kupata ujauzito, pima, pata tiba na jikinge kupata maradhi kwa usalama wa kichanga tumboni.

Ke, unaongezaje hisia zako za ngono?

Ke, unaongezaje hisia zako za ngono?

Mazoezi, kuacha msongo, maongezi na mwenza, kuweka manjonjo wakati wa tendo, kuacha tabia hatarishi na kula mlo wa kingono ni baadhi ya njia za kuchochea hisia za kufanya ngono kwa mwanamke.

Kiasi cha maji ya kunywa kila siku kwa watoto

Kiasi cha maji ya kunywa kila siku kwa watoto

Watoto wanapaswa kunywa maji vikombe 2 hadi 8 vya chai kwa siku huku wakiepushwa kutumia vinywaji vyenye sukari. Ni muhimu umpe kiasi hicho cha maji siku zote bila kujali majira ya mwaka, hata hivyo mahitaji ya maji huongezeka zaidi wakati wa mazoezi, homa ya kuharisha n.k.

Kiasi na siku za  kutokwa damu baada ya kutoa mimba kwa misoprostol

Kiasi na siku za kutokwa damu baada ya kutoa mimba kwa misoprostol

Kutokwa damu baada ya kutumia misoprostol hutegemea umri wa ujauzito, na kawaida hudumu kwa siku 3 hadi 14. Mgonjwa anapaswa kumuona daktari haraka akiona damu nyingi kupita kiasi, homa, maumivu makali au harufu mbaya.

bottom of page