top of page

Mwandishi;

Dkt. Mercy M, CO

Mhariri;

Dkt. Mangwella S, MD

19 Septemba 2021 14:27:28

Kirusi Rota B

Kirusi Rota B

Kirusi Rota B ni kirusi kinasababisha maambukizi kwenye mfumo wa chakula na kusababisha homa kali ya kuharisha na kutapika kwa watoto na watu wazima.


Kirusi Rota B kimeanza mwaka gani?


Tafiti zinaonesha kuwa kirusi Rota B kilionekana kwa mara ya kwanza mwaka 1982 uko China, kisha kikaonekana uko India mwaka 1998 na mwaka 2000 kikaonekana Bangladesh.


Kirusi Rota B kipo katika Familia gani?


Kirusi Rota B ni kimoja wapo kwenye genus ya kirusi Rota na familia ya Reoviridae. Virusi katika familia hii hufahamika kwa kuwa na strendi mbili ya RNA pia husababisha homa ya kuharisha na kutapika kwa watoto na watu wazima.


Sifa za kirusi


Rota B ni moja ya kirusi cha strendi mbili ya RNA. Kirusi hiki ni familia ya virusi vya Reoviridae.Familia hii ina sifa zifuatazo;


  • Wana RNA mbili 

  • Ana Strendi mbili ya RNA

  • Ukuta wa juu ya seli yake umefungwa na shelled capsid mbili

  • Wana umbile la ringi

  • Wana kipenyo chenye urefi wa 70nm

  • Genome yake ina vpande 11


Familia Reoviridae


Familia Reoviridae ina spishi tisa moja wapo akiwa kirusi rota A ambazo ni;


  • Kirusi rota A

  • Kirusi rota B

  • Kirusi rota C

  • Kirusi rota D

  • Kirusi rota E

  • Kirusi rota F

  • Kirusi rota G

  • Kirusi rota H

  • Kirusi rota I


Spishi Zinazosababisha ugonjwa kwa binadamu ni;


  • Kirusi Rota A

  • Kirusi Rota B

  • Kirusi rota C


Kirusi hutunzwa na nani?


Kirusi Rota A hutunzwa na binadamu.


Kirusi Rota B kinaenezwa kwa njia gani?


Kirusi Rota B kinaenezwa kwa njia zifuatazo;


  • Kula chakula kilichoandaliwa na mtu mwenye maambukizi ambaye hakunawa mikono yake baada ya kutoka chooni

  • Kutumia maji ya kunywa au chakula chenye vimelea

  • Kushikana mikono na mtu mwenye maambukizi ambaye hakunawa mikono baada ya kutoka chooni

  • Watoto kugusa sehemu chafu pia kupeleka mdomoni bila kunawa mikono


Vihatarishi vya kupata maambukizi ya kirusi Rota B


  • Mtu yeyote ambayo hajapata chanjo ya kirusi Rota

  • Watoto wadogo

  • Watu ambao umri umeenda sana

  • Watu wazima wanaolea watoto wenye maambukizi


Dalili za ugonjwa wa homa ya kuhara


Dalili za homa ya kuhara huonekana ndani ya siku mbili baada ya mtu kupata maambukizi ambazo ni;


  • Kuharisha choo chenye majimaji na wakati mwingine damu kidogo.

  • Kupata homa

  • Kutapika

  • Tumbo kuuma

  • Kukosa hamu ya kula

  • Mwili kukosa nguvu na kuchoka


Ishara mbaya zinazoweza kuonekana kwa mgonjwa;


  • Mdomo kukauka

  • Miungurumo ya tumbo kuongezeka

  • Macho kuingia ndani

  • Ngozi inapovutwa kurejea taratibu kwenye hali yake ya kawaida

  • Mapigo ya moyo kwenda kasi

  • Kupungua uzito


Vipimo vya kirusi Rota B


  • Picha nzima ya damu

  • Kiwango cha madini kwenye damu

  • Kipimo cha haja kubwa

  • Latex agglutination

  • Enzyme immune Assay

  • RT-PCR


Magonjwa yanayofana na Dalili za Rota B


Magonjwa yanayoweza kufanana dalili na homa ya matumbo ni pamoja na;


  • Giardiasis

  • Kuishiwa maji kwa mtoto

  • Gastroenteraitiz inayohitaji matibu ya dharura

  • Maambukizi ya salmonella kwa motto


Matibabu


Hakuna matibabu maalum kwa ajiri ya ugonjwa kuhara na kutapika kutokana na maambukizi ya kirusi rota B, ila mgonjwa anaweza pata yafuatayo;


  • Hakikisha njia ya hewa, upumuaji na mzunguko wa damu uko vizuri.

  • Mtoto atapatiwa ORS kwaajiri ya kunywa kama ana dalili kiasi au za wastani za kuishiwa maji au

  • Kuongezewa maji yenye madini sodium, potassium, chloride na calcium kwa njia ya mshipa kama ana upungufu mkali wa maji wilini

  • Mtoto anatakiwa apate muda mwingi wa kupumzika

  • Mtoto atapata panadol kwa ajiri ya maumivu na homa

  • Mtoto atapatiwa Zinc ya watoto ili kuharakisha uponyaji wa tumbo na kupunguza kuharisha

  • Mtoto atapatiwa dawa za kuzuia kutapika kama anatapika sana


Kinga


Fanya yafuatayo ili uweze kuwakinga wengine endapo umepata maambukizi;


  • Pata chanjo ya kirusi Rota A kwa wakati sahihi

  • Osha mikono yako mara kwa mara baada ya kugusa sehemu yoyote hasa mara baada ya kuingia na kutoka chooni

  • Nawa mikono ya watoto mara kwa mara kwa maji safi na sabuni

  • Zingatia usafi kwa ujumla


Chanjo


Je kuna chanjo ya kirusi Rota B? Chanjo kwa ajiri ya kirusi Rota B ipo. Kuna chanjo aina mbili ambazo ni Rotateq inatolewa kwa mtoto wa wiki 6 hadi 32 na Rotarix inatolewa kwa mtoto wa wiki 6 hadi 24.


ULY clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kuchukua hatua yoyote inayohusu afya yako


Wasiliana na daktari wa ULY clinin kwa ushauri na Tiba kwa kupiga nambza za simu au kubonyeza "Pata Tiba"chini ya tovuti hii

​

Orodha kuu


Rejea zamada hii;

  1. Takeshi Sanekata sanekata, et al. Human group B Rotavirus Infections Cause Severe Diarrhea in Children and Adult. https://journals.asm.org/doi/10.1128/JCM.41.5.2187-2190.2003. Imechukuliwa 17/09/2021. 

  2. MSD. Rota B virus. https://www.msdmanuals.com/professional/infectious-diseases/immunization/rotavirus-vaccine#v39242815. Imechukuliwa 17/09/2021. 

  3. Medscape. Rota B virus. https://emedicine.medscape.com/article/803885-overview. Imechukuliwa 17/09/2021. 

  4. Science direct. Rota B Virus. https://www.sciencedirect.com/topics/medicine-and-dentistry/rotavirus-b. Imechukuliwa 17/09/2021.

Imeboreshwa;

27 Septemba 2021 12:09:34

bottom of page