Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
Dkt. Mangwella S, MD
Dkt. Charles W, MD
24 Agosti 2026, 03:43:15

Chai ya rozela
Kunywa vikombe vitatu vya chai ya rozela hudhibiti mapigo ya moyo, hupunguza lehemu na mafuta yaliyoshamiri kwenye damu hivyo kulinda mishipa ya damu na kudhibiti kwa kiasi kikubwa shinikizo la juu la damu.
Namna ya kuandaa
Hatua ya kwanza:-Chemsha nusu kikombe cha rozela katika lita mbili za maji kwa muda wa dakika mbili
Hatua ya pili:-Acha ipoe kwa muda wa dakika 10 kisha chuja
Unaweza ongeza utamu kwa kuweka asali kijiko kimoja cha chai kwenye kila kikombe cha chai au kunywa bila sukari
Unaweza kunywa pia na familia yako au kuhifadhi kiasi kilichobaki kwenye jokofu
Faida za chai ya rozela
Hudhibiti mapigo ya moyo
Hukinga mishipa ya damu dhidi ya shinikizo la juu la damu na mafuta yaliyoshamiri
Huwa na lehemu kidogo
Hupunguza sumu ya oksijeni kwenye chembe hai
Humkinga mtu na kisukari
Hulinda ini
Hupunguza mzio
Soma zaidi kuhusu namna ya kuandaa chai hii na viungo vingine vinavyotakiwa kwenye makala za mlo wa kiafya
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 19:17:51
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
