Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
Dkt. Salome A, MD
Dkt. Benjamin L, MD
31 Oktoba 2026, 15:23:37

FEFO inafaida gani kwa mjamzito?
Jibu kwa ufupi
Jibu kwa ufupi: Meza FEFO kila siku katika ujauzito wote kama kliniki inavyoelekeza. Soma Umuhimu wa FEFO.
Maelezo
Faida za madini chuma
Huzuia upungufu wa damu wa mama – soma Upungufu wa damu wa madini chuma.
Hupunguza hatari ya mtoto kuzaliwa na uzito mdogo.
Mama huvumilia vizuri zaidi damu inayopotea wakati wa kujifungua.
Hupunguza uchovu na kizunguzungu.
Faida za folic acid
Huzuia mgongo wazi na kasoro nyingine za ubongo na uti wa mgongo.
Mrija wa fahamu wa mtoto hufunga ndani ya wiki 4 za kwanza – mara nyingi kabla mama hajajua ana mimba.
Ndiyo sababu wanaopanga mimba waanze folic acid miezi 1 hadi 3 kabla – soma Folic acid kabla na wakati wa ujauzito.
Nini cha kufanya
Meza kidonge kimoja kila siku kama ulivyoelekezwa kliniki.
Meza na maji au juisi ya machungwa; usimeze pamoja na chai, kahawa au maziwa – hupunguza ufyonzaji.
Choo kigumu au cheusi ni kawaida – kunywa maji, kula mboga; tumbo likiuma meza baada ya chakula au usiku.
Kula pia vyakula vyenye madini chuma – maini, nyama, dagaa, maharagwe, mboga za kijani.
Weka vidonge mbali na watoto – overdose ya madini chuma ni hatari kwa mtoto.
Dalili za hatari
Kuchoka sana, kupumua kwa shida, moyo kwenda mbio au kuzimia – nenda kituo cha afya mara moja; soma Dalili za upungufu wa damu.
Lini umwone daktari
Huwezi kumeza FEFO kwa sababu ya kichefuchefu au kutapika.
Viganja, kope na midomo kuwa vyeupe.
Una ugonjwa wa seli mundu – ushauri maalumu wa madini chuma.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
1. FEFO inatibu nini?
Huzuia na kutibu upungufu wa damu, na kuzuia mgongo wazi kwa mtoto.
2. FEFO inaleta choo cheusi?
Ndiyo, ni kawaida.
3. Nimeze FEFO na chai?
Hapana, chai hupunguza ufyonzaji; tumia maji au juisi.
4. Nianze FEFO lini?
Mara tu unapoanza kliniki; folic acid ni bora hata kabla ya mimba.
5. FEFO inanikichefua, niache?
Usiache – meza baada ya chakula au usiku; ongea na kliniki.
6. Nikimeza FEFO mtoto atakuwa mkubwa sana?
Hapana, haiongezi ukubwa wa mtoto kupita kiasi.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 19:07:23
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
Ministry of Health, United Republic of Tanzania. Standard Treatment Guidelines and National Essential Medicines List (STG/NEMLIT), 7th edition. Dodoma: Ministry of Health; 2026.
World Health Organization. WHO recommendations on antenatal care for a positive pregnancy experience. Geneva: WHO; 2016.
De-Regil LM, et al. Effects and safety of periconceptional oral folate supplementation for preventing birth defects. Cochrane Database Syst Rev. 2015;(12):CD007950.

