top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

Dkt. Lusenge S,MD

Dkt. Sospeter M, MD

2 Aprili 2026, 16:17:51

Umuhimu wa FEFO

FEFO  ni dawa yenye mchanganyiko wa virutubisho vya madini chuma na folic acid. Dawa hii ipo katika kundi la dawa za kuongeza damu mwilini.


Husaidia kutibu na kuzuia upungufu wa damu unaosababishwa na upungufu wa madini chuma na folic acid.

Kwa wajawazito husaidia kuzuia hatari ya upungufu wa damu na madhara yake kama vile kujifungua kabla ya mimba kukomaa, kujifungua njiti, kutokwa damu nyingi wakati wa kujifungua.


Folic acid katika dawa hii huzuia maradhi katika mfumo wa fahamu wa mtoto, maradhi hayo ni kama mgongo wazi na ubongo wazi


Nini unapaswa kufahamu zaidi?

Virutubishi katika dawa ya FEFO hupatikana katika vyakula kama mboga za majani, karanga, nyama nk. Ulaji wa vyakula hivi husaidia kuzuia upungufu wa damu.


Wapi unapata maelezo zaidi?

Kwa maelezo zaidi soma makala ya umuhimu wa folic acid kwa mjamzito

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 16:17:51

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

​

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

bottom of page