Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
Dkt. Benjamin L, M.D
Dkt. Peter A, M.D
31 Oktoba 2026, 15:23:37

Je, kiwango cha kawaida cha manii ni ngapi?
Jibu kwa ufupi
Jibu kwa ufupi: Manii milioni 16 au zaidi kwa mililita ni kawaida. Kipimo kimoja hakitoshi – kama si cha kawaida, hurudiwa baada ya wiki chache. Soma Ugumba.
Maelezo
Viwango vya chini vya kawaida (WHO 2021)
Kiasi cha shahawa – mililita 1.4.
Idadi kwa mililita – milioni 16.
Jumla kwa bao – milioni 39.
Wanaotembea (jumla) – asilimia 42; wanaosonga mbele – asilimia 30.
Umbo la kawaida – asilimia 4.
Walio hai – asilimia 54.
Kinachoathiri idadi
Kumwaga siku 1 iliyopita au zaidi ya siku 7 – kipimo hufanywa baada ya siku 2 hadi 7 bila kumwaga.
Homa ya karibuni (miezi 3).
Sigara, pombe, bangi, steroidi za mazoezi.
Joto kali kwenye korodani, varicocele, maambukizi.
Uzito mkubwa, kisukari, homoni.
Nini cha kufanya
Kipimo kisicho cha kawaida – rudia baada ya wiki 4 hadi 12.
Acha sigara, punguza pombe, dumisha uzito, epuka joto kwenye korodani.
Lishe bora – soma Zinki na manii.
Pimeni wote wawili – soma Mambo ya kufanya endapo hushiki mimba.
Dalili za hatari
Korodani kuvimba ghafla na kuuma – hospitali mara moja.
Lini umwone daktari
Hamjapata mimba mwaka 1.
Kipimo kinaonyesha manii chache au hakuna kabisa.
Korodani ndogo, uvimbe kwenye korodani, au historia ya matumbwitumbwi.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
1. Manii milioni 10 kwa mililita naweza kumpa mimba mke wangu?
Inawezekana, ingawa nafasi ni ndogo zaidi; rudia kipimo na mwone mtaalamu.
2. Kiasi kidogo cha shahawa ni tatizo?
Chini ya mililita 1.4 kinahitaji uchunguzi.
3. Nifanyeje kabla ya kipimo cha manii?
Usimwage kwa siku 2 hadi 7 kabla.
4. Uzito mkubwa unapunguza manii?
Ndiyo, unaweza.
5. Manii yanachukua muda gani kujirudia?
Karibu miezi 3 – mabadiliko ya maisha huonekana baada ya hapo.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 19:07:23
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
World Health Organization. WHO laboratory manual for the examination and processing of human semen. 6th ed. Geneva: WHO; 2021.
Leslie SW, Soon-Sutton TL, Khan MA. Male infertility. StatPearls. 2024.

