top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

ULY CLINIC

31 Oktoba 2026, 15:23:37

Je mtoto wa miezi 4 anapaswa kula nini?

Jibu kwa ufupi


Jibu kwa ufupi: Maziwa ya mama pekee hadi miezi 6. Soma Uji kabla ya miezi 6.


Maelezo


Maziwa ya mama


  • Yana virutubisho vyote na maji ya kutosha – hata wakati wa joto.

  • Humkinga mtoto dhidi ya maambukizi.

  • Nyonyesha mara 8 hadi 12 kwa siku au zaidi – soma Namna nzuri ya kunyonyesha.


Mama akirudi kazini



Asipewe


  • Uji, maji, chai, juisi, matunda, vyakula vya familia, dawa za kienyeji.


Nini cha kufanya


  • Formula pale tu maziwa ya mama hayawezekani – changanya kama maelekezo.

  • Usimpe maziwa ya ng'ombe kabla ya miezi 6.

  • Pima uzito kila mwezi kliniki.


Dalili za hatari


Mpeleke kituo cha afya mara moja ukiona:


  • Hanyonyi, analegea.

  • Kuharisha au kutapika kila anachonyonya.

  • Hakojoi angalau mara 6 kwa siku.


Lini umwone daktari


  • Uzito hauongezeki.

  • Unadhani maziwa yako hayatoshi.


Maswali yanayoulizwa mara kwa mara


1. Mtoto wa miezi 4 anaweza kunywa maji?

Hapana, maziwa ya mama yanatosha.

2. Nimpe uji kidogo akionekana na njaa?

Hapana – mnyonyeshe mara nyingi zaidi.

3. Formula inafaa kwa miezi 4?

Ndiyo, kama maziwa ya mama hayawezekani.

4. Mtoto aanze chakula lini?

Akitimiza miezi 6.

5. Maziwa yangu ni machache, nifanyeje?

Nyonyesha mara nyingi zaidi, kunywa maji, kula vizuri; mwone mtoa huduma.

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 17:07:17

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

​

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

Rejea za mada hii:

  1. Ministry of Health, United Republic of Tanzania. Standard Treatment Guidelines and National Essential Medicines List (STG/NEMLIT), 7th edition. Dodoma: Ministry of Health; 2026.

  2. World Health Organization. Infant and young child feeding – fact sheet. Geneva: WHO; 2023.

bottom of page