Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
Dkt. Helen L, M.D
31 Oktoba 2026, 15:23:37

Jifunze tabia tano za kiafya
Jibu kwa ufupi
Jibu kwa ufupi: Kifungua kinywa chenye protini na nafaka, matunda na mboga kila mlo, nafaka zisizokobolewa, mafuta ya mimea kwa kiasi, na kutembea dakika 30 kwa siku. Soma Epuka unene.
Maelezo
1. Kifungua kinywa
Mfano: uji wa ulezi au mtama, mayai, maharage, mkate wa ngano isiyokobolewa, maziwa mgando, tunda.
Kifungua kinywa hakijaonyesha kupunguza uzito peke yake, lakini husaidia kupata virutubisho na nguvu.
2. Matunda na mboga
Angalau mara 5 kwa siku (gramu 400).
Tunda zima ni bora kuliko juisi – lina nyuzilishe na sukari kidogo inayofyonzwa.
Mboga za majani kila mlo: mchicha, matembele, majani ya maboga.
3. Nafaka zisizokobolewa
Dona, ulezi, mtama, uwele, mchele wa kahawia, mkate wa ngano isiyokobolewa – nyuzilishe huzuia choo kigumu na sukari kupanda haraka.
4. Mafuta yenye afya
Mafuta ya mimea (alizeti, karanga, mzeituni) na samaki, kwa kiasi.
Punguza samli, mafuta ya nyama, mafuta yaliyotumika mara nyingi na vyakula vya kukaanga.
Mafuta ya mimea hayana kolestrol, lakini mafuta mengi ya aina yoyote huongeza uzito.
5. Mazoezi
Dakika 150 kwa wiki – kutembea haraka, kuendesha baiskeli, kucheza.
Mazoezi ya nguvu siku 2 kwa wiki.
Punguza kukaa muda mrefu.
Nini cha kufanya
Anza na tabia moja wiki hii.
Weka matunda mezani badala ya biskuti.
Tembea au panda ngazi badala ya lifti.
Soma Siri za afya ya akili.
Dalili za hatari
Maumivu ya kifua au kushindwa kupumua wakati wa mazoezi – acha na nenda hospitali.
Lini umwone daktari
Una presha, kisukari au ugonjwa wa moyo na unaanza mazoezi makali.
Uzito unaongezeka licha ya mabadiliko.
Hujapima presha, sukari na lehemu kwa zaidi ya mwaka.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
1. Kifungua kinywa kinapunguza uzito?
Si peke yake, lakini ni mlo mzuri wa virutubisho.
2. Juisi au tunda zima?
Tunda zima ni bora.
3. Mafuta gani ni bora?
Ya mimea na samaki, kwa kiasi.
4. Mafuta ya alizeti yana kolestrol?
Hapana, lakini yatumike kwa kiasi.
5. Mazoezi kiasi gani?
Dakika 150 kwa wiki.
6. Nafaka zisizokobolewa ni zipi?
Dona, ulezi, mtama, uwele, mchele wa kahawia.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 19:17:50
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
World Health Organization. Healthy diet fact sheet. Geneva: WHO; 2020.
World Health Organization. Guideline: sugars intake for adults and children. Geneva: WHO; 2015.
World Health Organization. WHO guidelines on physical activity and sedentary behaviour. Geneva: WHO; 2020.
Sievert K, et al. Effect of breakfast on weight and energy intake: systematic review and meta-analysis of randomised controlled trials. BMJ. 2019;364:l42.
Pamplona-Roger GD. Encyclopedia of Foods and Their Healing Power. Vol. 1. Education and Health Library; 2004.

