top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

ULY CLINIC

31 Oktoba 2026, 15:23:37

Kikokotoo cha uzito wa mtoto miezi 0 hadi 24: Uzito wa kawaida na usio wa kawaida

Jibu kwa ufupi


Jibu kwa ufupi: Tumia kikokotoo kufuatilia ukuaji kati ya mahudhurio ya kliniki. Matokeo ya uzito mdogo sana au mkubwa sana – nenda kliniki apimwe vizuri.



Maelezo


Jinsi ya kutumia


  • Chagua jinsia – kiume au kike.

  • Weka umri kwa miezi – unaweza kuweka nusu mwezi (mfano 6.5).

  • Weka uzito kwa kilo – mfano 7.2.

  • Bonyeza Hesabu.


Kusoma matokeo


  • Chini ya -3 SD – uzito mdogo sana; uchunguzi wa haraka.

  • -3 hadi -2 SD – uzito mdogo; ushauri wa lishe na ufuatiliaji.

  • -2 hadi +2 SD – kawaida.

  • Zaidi ya +2 SD – uzito mkubwa; ushauri wa lishe.


Mambo ya kujua


  • Mstari wa ukuaji kupanda kila mwezi ni muhimu kuliko kipimo kimoja.

  • Mtoto mfupi kwa urefu anaweza kuwa na uzito mdogo bila kukonda.

  • Utapiamlo mkali hugunduliwa kwa uzito-kwa-urefu, MUAC (kipimo cha mkono) na uvimbe wa miguu yote.

  • Mizani isiyo sahihi au mtoto amevaa nguo nzito hubadilisha matokeo.


Nini cha kufanya


  • Pima uzito kliniki kila mwezi na linganisha na kadi ya ukuaji.

  • Uzito mdogo – ongeza milo na chakula cha wanyama; soma Uzito mdogo kwa mtoto wa miezi 9, Mlo wa miezi 9 na Mlo wa miezi 6.

  • Uzito mkubwa – endelea kunyonyesha, punguza vinywaji vya sukari na vyakula vya kukaanga.

  • Kikokotoo si mbadala wa kliniki.


Dalili za hatari


Mpeleke kituo cha afya mara moja ukiona:


  • Miguu yote imevimba.

  • Amekonda sana – mbavu wazi, ngozi imelegea.

  • Hali wala hanyonyi, analegea.

  • Kuharisha au kutapika kila kitu.


Lini umwone daktari


  • Matokeo ni chini ya -2 SD au zaidi ya +2 SD.

  • Uzito haupandi mwezi 2 mfululizo.

  • Uzito unashuka.


Maswali yanayoulizwa mara kwa mara


1. Mtoto wa miezi 6 ana kilo 6, ni kawaida?

Weka kwenye kikokotoo kwa jinsia yake; kwa wengi kiko karibu na kiwango cha chini cha kawaida – fuatilia kliniki.

2. SD ina maana gani?

Inaonyesha umbali wa uzito wa mtoto kutoka wastani wa watoto wa umri wake.

3. Uzito mdogo sana ni utapiamlo mkali?

Si lazima. Kliniki hupima pia urefu, MUAC na uvimbe wa miguu.

4. Mtoto mnene ni mwenye afya zaidi?

Hapana, uzito mkubwa kupita kiasi pia si mzuri.

5. Nipime uzito mara ngapi?

Kila mwezi kliniki hadi miaka 2.

6. Kikokotoo kinafaa kwa mtoto njiti?

Tumia umri uliorekebishwa (umri ukitoa wiki alizowahi) kwa ushauri wa mtoa huduma.

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 17:07:37

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

​

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

Rejea za mada hii:

  1. World Health Organization. WHO child growth standards: length/height-for-age, weight-for-age, weight-for-length, weight-for-height and BMI-for-age. Geneva: WHO; 2006.

  2. World Health Organization. Guideline on the prevention and management of wasting and nutritional oedema in infants and children under 5 years. Geneva: WHO; 2023.

bottom of page