top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

Dkt. Benjamin L, MD

31 Oktoba 2026, 15:23:43

Kinyesi kwa kichanga: Mwongozo kwa Wazazi

Jibu kwa ufupi


Jibu kwa ufupi: Mara 1–6+ kwa siku, njano-kijani, kamasi kidogo – kawaida kama ananyonya vizuri na kuongezeka uzito. Nyeupe/kijivu, damu, kutapika kijani, homa – hospitali leo. Soma Muundo na rangi ya haja ya kichanga.


Maelezo


Kawaida


  • Mara 1–6+ kwa siku.

  • Njano, kijani, kahawia.

  • Laini/majimaji, mbegu.

  • Kamasi kidogo mara moja moja.

  • Kijani – soma Kinyesi cha kijani.


Choo kigumu kweli


  • Kigumu kama vijiwe.

  • Kulia sana anapojisaidia.

  • Tumbo kuvimba.

  • Nadra kwa anayenyonya pekee.


Nini cha kufanya


  • Nyonyesha mara nyingi.

  • Hesabu nepi za mkojo (6+).

  • Pima uzito kliniki.

  • Usimpe maji, chai wala dawa za tumbo.


Dalili za hatari


Hospitali leo mtoto akiwa na:


  • Kinyesi cheupe/kijivu – soma Rangi ya kinyesi.

  • Damu.

  • Kutapika kijani, tumbo kuvimba.

  • Homa, kutonyonya, kulegea.

  • Majimaji mengi na macho kuingia ndani.


Lini umwone daktari


  • Haongezeki uzito.

  • Kinyesi kigumu mara kwa mara.

  • Kamasi nyingi kila siku.


Maswali yanayoulizwa mara kwa mara


1. Mara 6 kwa siku ni nyingi?

Kawaida kwa anayenyonya.

2. Kamasi kidogo?

Kawaida mara moja moja.

3. Siku 3 bila haja (wiki 6)?

Kawaida kama ni laini.

4. Kijani ni ugonjwa?

Mara nyingi hapana.

5. Nimpe maji?

Hapana kabla ya miezi 6.

6. Lini hospitali?

Nyeupe, damu, homa, kutapika kijani.

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 19:07:08

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

​

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

Rejea za mada hii:

  1. Den Hertog J, et al. The defecation pattern of healthy term infants up to the age of 3 months. Arch Dis Child Fetal Neonatal Ed. 2012;97(6):F465–70.

  2. Tabbers MM, et al. Evaluation and treatment of functional constipation in infants and children: ESPGHAN and NASPGHAN recommendations. J Pediatr Gastroenterol Nutr. 2014;58(2):258–74.

  3. World Health Organization. Pocket book of hospital care for children. 2nd ed. Geneva: WHO; 2013.

bottom of page