top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

ULY CLINIC

31 Oktoba 2026, 15:23:37

Kipimo cha mimba kwa mkojo- Kikokotoo cha kutafsiri majibu

Jibu kwa ufupi


Jibu kwa ufupi: Weka tarehe ya kwanza ya hedhi ya mwisho na urefu wa mzunguko, bonyeza 'Angalia Matokeo'. Pima kwa mkojo wa asubuhi siku hedhi ilipotarajiwa au baadaye.



Maelezo


Kutafsiri majibu


  • Mistari 2 (hata hafifu) – chanya; mimba ipo mara nyingi.

  • Mstari 1 (wa kudhibiti) – hasi; kama hedhi bado haijaja, rudia baada ya siku 7.

  • Hakuna mstari wa kudhibiti – kipimo kimeharibika; tumia kingine.

  • Soma majibu ndani ya muda ulioandikwa – mistari inayotokea baadaye haiaminiki.


Hasi ya uongo


  • Kupima mapema mno.

  • Mkojo mwepesi baada ya kunywa maji mengi.

  • Mzunguko mrefu au uovuleshaji ulichelewa.


Chanya ya uongo (nadra)



Nini cha kufanya


  • Tumia mkojo wa kwanza wa asubuhi.

  • Fuata maelekezo ya kipimo; angalia tarehe ya mwisho ya matumizi.

  • Chanya – anza kliniki mapema; folic acid.

  • Hasi lakini hedhi haiji wiki 3 – mwone mtoa huduma.


Dalili za hatari



Lini umwone daktari


  • Majibu yanachanganya mara 2.

  • Hedhi haijaja miezi 3 na kipimo ni hasi.


Maswali yanayoulizwa mara kwa mara


1. Nipime mimba lini?

Siku hedhi ilipotarajiwa au baadaye.

2. Mstari hafifu ni chanya?

Ndiyo, mara nyingi.

3. Kwa nini kipimo ni hasi lakini sijaona hedhi?

Huenda umepima mapema; rudia baada ya siku 7.

4. Mkojo wa saa ngapi ni bora?

Wa kwanza asubuhi.

5. Kipimo kinaweza kuwa chanya baada ya mimba kutoka?

Ndiyo, hadi wiki 3 hadi 4.

6. Kikokotoo kinathibitisha mimba?

Hapana, kinakusaidia kupima wakati sahihi.

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 19:07:21

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

​

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

Rejea za mada hii:

  1. Wilcox AJ, et al. Natural limits of pregnancy testing in relation to the expected menstrual period. JAMA. 2001;286(14):1759–61.

  2. Gronowski AM, et al. False-negative results in point-of-care qualitative hCG devices due to excess hCGβ core fragment. Clin Chem. 2009;55(7):1389–94.

  3. Cole LA. hCG, the wonder of today's science. Reprod Biol Endocrinol. 2012;10:24.

bottom of page