Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
Dkt. Benjamin L, MD, Dkt. Adolf S, MD
31 Oktoba 2026, 15:23:37

Kipindi cha kwanza cha ujauzito
Jibu kwa ufupi
Jibu kwa ufupi: Kliniki kabla ya wiki 12, folic acid kila siku, hakuna pombe wala sigara, usitumie dawa bila ushauri. Damu au maumivu makali – hospitali. Soma Folic acid kabla na wakati wa ujauzito.
Maelezo
Ukuaji wa mtoto (wiki kutoka hedhi ya mwisho)
Wiki 5–6 – mrija wa fahamu (ubongo, uti wa mgongo), moyo huanza kupiga.
Wiki 7–8 – mikono, miguu, macho, masikio huanza.
Wiki 10 – viungo vyote vikuu vimeanza; urefu karibu sm 3.
Wiki 11–13 – kucha, kope, kisanduku cha sauti; mtoto hucheza lakini mama hahisi bado – soma Kucheza kwa mtoto tumboni.
Kliniki ya kwanza
Historia, presha, uzito.
Damu (Hb, kundi la damu), VVU, kaswende, homa ya ini B, mkojo.
Ultrasound kuthibitisha umri wa mimba.
Folic acid na chuma; chanjo ya pepopunda.
WHO hushauri angalau mikutano 8 ya kliniki.
Vinavyoweza kudhuru mtoto
Pombe, sigara, dawa za kulevya.
Baadhi ya dawa – za chunusi (isotretinoin), kifafa (valproate), warfarin, baadhi ya dawa za presha (ACE inhibitors).
Maambukizi – rubella, kaswende, toxoplasma.
Mionzi isiyo ya lazima.
Nini cha kufanya
Folic acid kila siku hadi wiki 12, kisha pamoja na chuma.
Kula kidogo mara nyingi kwa kichefuchefu.
Lala kwenye chandarua.
Mweleze kila mtoa huduma kuwa una mimba kabla ya dawa au X-ray.
Dalili za hatari
Hospitali mara moja ukiwa na:
Damu ukeni na maumivu ya tumbo.
Maumivu makali upande mmoja, kizunguzungu, kuzimia.
Kutapika kila kitu, kushindwa kunywa.
Homa kali.
Lini umwone daktari
Hujaanza kliniki kufikia wiki 12.
Unatumia dawa za kudumu (kifafa, presha, kisukari, VVU) – usiache, mwone mtoa huduma.
Kuwashwa kukojoa au uchafu ukeni.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
1. Kipindi cha kwanza ni wiki ngapi?
Wiki 1 hadi 13.
2. Moyo wa mtoto huanza lini?
Karibu wiki ya 6.
3. Nianze kliniki lini?
Kabla ya wiki 12.
4. Folic acid ni muhimu?
Ndiyo, huzuia ulemavu wa uti wa mgongo.
5. Naweza kutumia dawa yoyote?
Hapana; uliza mtoa huduma kwanza.
6. Kichefuchefu huisha lini?
Mara nyingi kufikia wiki 14–16.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 19:17:51
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
​
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
World Health Organization. WHO recommendations on antenatal care for a positive pregnancy experience. Geneva: WHO; 2016.
Moore KL, Persaud TVN, Torchia MG. The Developing Human: Clinically Oriented Embryology. 11th ed. Philadelphia: Elsevier; 2019.
American College of Obstetricians and Gynecologists. How your fetus grows during pregnancy. FAQ156. Washington, DC: ACOG; 2024.
Ministry of Health, United Republic of Tanzania. Standard Treatment Guidelines and National Essential Medicines List (STG/NEMLIT), 7th edition. Dodoma: Ministry of Health; 2026.

