top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

ULY CLINIC

31 Oktoba 2026, 15:23:37

Kuchelea kwa hedhi baada ya norethisterone shida ni nini?

Jibu kwa ufupi


Swali la mteja: "Habari daktari, nimetumia norethisterone, lakini sasa ni mwezi sioni hedhi. Ni kawaida au ni shida?"


Jibu kwa ufupi: Pima mimba sasa. Kama ni hasi na hedhi haijaja wiki 2 baadaye, mwone mtoa huduma. Soma Norethisterone na hedhi.


Maelezo


Kinachotarajiwa


  • Ukimeza kuchelewesha hedhi – hedhi huja siku 2 hadi 3 baada ya kuacha.

  • Ukimeza kutibu damu nyingi – hedhi ya kuacha inaweza kuwa nzito kidogo.

  • Mzunguko unaofuata unaweza kuwahi au kuchelewa kidogo.


Kwa nini hedhi inaweza isije


  • Mimba – kama ulifanya ngono bila kinga kabla au wakati wa dawa.

  • Uovuleshaji kuchelewa – mzunguko kubadilika baada ya homoni.

  • PCOS, tezi ya shingo, prolaktini juu, msongo, kupungua uzito – soma Kwa nini piriodi imesimama?.

  • Ulikuwa hupati hedhi tangu mwanzo – tatizo la awali halijatibiwa.


Nini cha kufanya


  • Pima mimba kwa mkojo; kama hasi, rudia baada ya siku 7.

  • Usimeze norethisterone tena 'kurudisha hedhi' bila uchunguzi.

  • Norethisterone si uzazi wa mpango – tumia kondomu au njia nyingine.

  • Andika tarehe ulizomeza dawa na za hedhi kwa mtoa huduma.

  • Soma Dawa ya kukata hedhi na Hedhi kuchelewa.


Dalili za hatari


Nenda kituo cha afya mara moja ukiwa na:


  • Kipimo chanya na maumivu makali upande mmoja wa tumbo.

  • Maumivu na kuvimba kwa mguu mmoja, au maumivu ya kifua ghafla ukiwa kwenye dawa.


Lini umwone daktari


  • Hedhi haijaja wiki 2 baada ya kuacha dawa na kipimo ni hasi.

  • Hedhi haijaja miezi 3.

  • Damu nzito au isiyo na mpangilio inarudi.


Maswali yanayoulizwa mara kwa mara


1. Hedhi huja lini baada ya kuacha norethisterone?

Mara nyingi siku 2 hadi 3, wakati mwingine hadi wiki 1.

2. Norethisterone inazuia mimba?

Hapana, kwa jinsi inavyotumika kuchelewesha hedhi.

3. Mwezi umepita sijaona hedhi, nifanyeje?

Pima mimba, kisha mwone mtoa huduma.

4. Norethisterone inaweza kutoa mimba?

Hapana.

5. Nimeze tena ili hedhi irudi?

Si bila uchunguzi wa mtoa huduma.

6. Norethisterone inaweza kuvuruga mzunguko?

Ndiyo, kwa mwezi mmoja au miwili.

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 19:07:15

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

​

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

Rejea za mada hii:

  1. Medicines and Healthcare products Regulatory Agency. Norethisterone 5 mg tablets – Summary of Product Characteristics. London: eMC; 2022.

  2. ACOG Practice Bulletin No. 222: Amenorrhea. Obstet Gynecol. 2020;136(4):e111–22.

bottom of page