Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
Dr.Sospeter Mangwella, MD
ULY CLINIC
31 Oktoba 2026, 15:23:37
Kwa nini piriodi imesimama?
Jibu kwa ufupi
Jibu kwa ufupi: Pima mimba kwanza. Kama si mimba na hedhi haijaja miezi 3, mwone mtoa huduma kwa vipimo. Soma Hedhi kuchelewa.
Maelezo
Visababishi vya kawaida
Mimba, kunyonyesha, komahedhi – soma Komahedhi na dalili zake.
Uzazi wa mpango – sindano, kipandikizi, kitanzi cha homoni; soma Kukosa hedhi baada ya sindano.
Msongo, kupungua uzito sana, mazoezi makali, ugonjwa mkubwa.
Visababishi vya homoni na maumbile
PCOS – hedhi chache, chunusi, nywele nyingi, uzito.
Tezi ya shingo – kufanya kazi kidogo au kupita kiasi.
Prolaktini juu – maziwa matitini bila kunyonyesha; uvimbe mdogo wa tezi ya ubongo au dawa.
Makovu ndani ya kizazi (Asherman) – baada ya kusafishwa kizazi au maambukizi.
Ovari kuchoka mapema – kabla ya miaka 40; soma Hedhi kukoma kabla ya miaka 45.
Dawa – soma Dawa zinazobadilisha hedhi.
Nini cha kufanya
Pima mimba; kama hasi na bado hakuna hedhi, rudia baada ya siku 7.
Andika tarehe za hedhi zilizopita, uzito, dawa unazotumia.
Kula vizuri; epuka kupunguza uzito haraka.
Usitumie dawa za 'kurudisha hedhi' bila uchunguzi.
Vipimo anavyoweza kuagiza mtoa huduma: homoni ya tezi, prolaktini, FSH, ultrasound.
Dalili za hatari
Nenda kituo cha afya mara moja ukiwa na:
Kipimo cha mimba chanya na maumivu makali upande mmoja.
Kichwa kuuma sana na kuona vibaya pamoja na hedhi kukoma.
Lini umwone daktari
Hedhi haijaja miezi 3 (au miezi 6 kama mzunguko wako hauna mpangilio).
Maziwa yanatoka matitini.
Nywele nyingi usoni, chunusi, uzito kuongezeka.
Joto la ghafla na jasho usiku kabla ya miaka 40.
Hukuwahi kuona hedhi kufikia miaka 15.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
1. Hedhi imesimama miezi 2, ni tatizo?
Pima mimba; kama hasi na haijaja miezi 3, mwone mtoa huduma.
2. Msongo wa mawazo unaweza kusimamisha hedhi?
Ndiyo.
3. Kupungua uzito kunasimamisha hedhi?
Ndiyo, hasa ukipungua sana au kwa haraka.
4. PCOS inaleta hedhi kusimama?
Ndiyo, au kuja mara chache.
5. Nikiacha sindano hedhi itarudi lini?
Inaweza kuchukua hadi karibu mwaka.
6. Nimeze dawa ya kurudisha hedhi?
Si kabla ya kujua chanzo; pima mimba kwanza.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 17:08:31
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
ACOG Practice Bulletin No. 222: Amenorrhea. Obstet Gynecol. 2020;136(4):e111–22.
Practice Committee of the American Society for Reproductive Medicine. Current evaluation of amenorrhea. Fertil Steril. 2008;90(5 Suppl):S219–25.
Ministry of Health, United Republic of Tanzania. Standard Treatment Guidelines and National Essential Medicines List (STG/NEMLIT), 7th edition. Dodoma: Ministry of Health; 2026.

