Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
Dkt. Sospeter B, MD
Dkt. Salome A, MD
31 Oktoba 2026, 15:23:37

Matibabu ya maumivu ya koo
Jibu kwa ufupi
Jibu kwa ufupi: Maumivu mengi ya koo hutibika nyumbani. Mwone mtoa huduma ukiwa na homa kali, usaha kwenye mafindofindo bila kikohozi, au maumivu zaidi ya wiki 1 – hasa watoto, kwa sababu strep isiyotibiwa huweza kuleta homa ya baridi yabisi inayoharibu moyo.
Maelezo
Aina kulingana na sehemu iliyoathirika
Koromeo (pharyngitis) – koo kuuma na kuwasha.
Mafindofindo (tonsillitis) – mafindofindo kuvimba, wakati mwingine usaha; soma Uvimbe wa mafindofindo.
Zoloto (laryngitis) – sauti kukwaruza au kupotea.
Viashiria
Koo kukwanguliwa, kuungua, kukauka, kukereketa.
Maumivu ukimeza au koo likishikwa.
Usaha au mabaka meupe kwenye koo.
Visababishi vingine: hewa kavu, kucheua tindikali, moshi, mzio, fangasi – soma Fangasi na maumivu ya koo.
Tiba ya nyumbani
Pumzika ili mwili upambane na maambukizi.
Sukutua maji ya uvuguvugu yenye chumvi kijiko 1 kwa kikombe 1 (robo lita) cha maji, mara kadhaa kwa siku.
Vinywaji vya uvuguvugu – chai yenye asali, supu, maji ya moto yenye limao.
Vitu baridi kama barafu hupooza koo kwa baadhi ya watu.
Ongeza unyevu chumbani kama hewa ni kavu.
Pumzisha sauti – hasa waimbaji na wazungumzaji.
Chai ya tangawizi, limao na asali, au chai ya chamomile.
Mchanganyiko wa magadi soda, limao na asali
Chota kiasi kidogo cha unga wa magadi soda (karibu moja ya nane ya kijiko cha chai) na weka kwenye kikombe.
Kamua limao au ndimu moja kubwa; subiri povu liishe.
Ongeza vijiko 2 vya asali, changanya, kisha kunywa.
Mara 2 kwa siku kwa siku 2 tu.
Usimpe mtoto chini ya mwaka 1 (asali); wenye vidonda vya tumbo, presha au ugonjwa wa figo waulize kwanza.
Nini cha kufanya
Dawa za maumivu kama paracetamol kwa ushauri wa mfamasia.
Usinunue antibiotiki bila kupimwa.
Ukipewa antibiotiki kwa strep, maliza dozi yote.
Usivute sigara; epuka moshi.
Soma pia Koo kuwasha kwa muda mrefu na Maumivu na kukauka kwa koo.
Dalili za hatari
Nenda hospitali mara moja ukiwa na:
Kupumua kwa shida au sauti ya kukoroma ukivuta pumzi.
Kushindwa kumeza hata mate – mate kutiririka.
Mdomo kushindwa kufunguka, sauti kama mtu mwenye kitu mdomoni, maumivu makali upande mmoja – jipu la koo.
Shingo kuvimba au kukakamaa.
Upele mwekundu kama msasa pamoja na koo kuuma.
Lini umwone daktari
Maumivu zaidi ya wiki 1, au yanajirudia mara nyingi.
Homa kali na usaha kwenye mafindofindo bila kikohozi.
Sauti kukwaruza zaidi ya wiki 3, hasa wavuta sigara – soma Kumeza kwa shida.
Koo kuuma hadi masikioni – soma Koo kuwaka moto mpaka masikioni.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
1. Koo linauma na nina mafua, nimeze antibiotiki?
Mara nyingi hapana – ni virusi, hupona kwa siku 3 hadi 7.
2. Maji ya chumvi yanasaidia koo?
Ndiyo, kusukutua maji ya uvuguvugu yenye chumvi hupunguza maumivu.
3. Mtoto wangu ana koo kuuma na homa kali, nifanyeje?
Mpeleke kituo cha afya apimwe – strep isiyotibiwa inaweza kuathiri moyo.
4. Barafu inaongeza maumivu ya koo?
Kwa wengi hupooza; kama inakuzidishia, tumia vinywaji vya uvuguvugu.
5. Mchanganyiko wa magadi na limao unafaa kwa kila mtu?
Hapana – si kwa watoto chini ya mwaka 1, na wenye vidonda vya tumbo, presha au figo waulize kwanza.
6. Kwa nini koo linauma asubuhi tu?
Mara nyingi hewa kavu, kupumua kwa mdomo au tindikali kupanda usiku.
Imeandikwa:
24 Agosti 2026, 03:58:14
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
Ministry of Health, United Republic of Tanzania. Standard Treatment Guidelines and National Essential Medicines List (STG/NEMLIT), 7th edition. Dodoma: Ministry of Health; 2026.
Brinckmann J, et al. Safety and efficacy of a traditional herbal medicine (Throat Coat) in symptomatic temporary relief of pain in patients with acute pharyngitis. J Altern Complement Med. 2003;9(2):285–98.
National Institute for Health and Care Excellence. Sore throat (acute): antimicrobial prescribing. NICE guideline NG84. 2018.

