Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
Dkt. Mercy M, M.D
Dkt. Mangwella S, MD
31 Oktoba 2026, 15:23:37

Matibabu ya presha pasipo dawa
Jibu kwa ufupi
Jibu kwa ufupi: Punguza chumvi, kula mboga na matunda kila mlo, punguza uzito, tembea dakika 30 siku nyingi, punguza pombe, acha sigara – na pima presha mara kwa mara. Soma Shinikizo la juu la damu.
Maelezo
Njia na kiasi cha kushusha (wastani)
DASH – mmHg 8–11.
Chumvi <5 g/siku – mmHg 5–6; epuka supu za pakiti, cubes, soseji, chipsi zenye chumvi; soma Chumvi na insulini.
Kupunguza uzito – karibu mmHg 1 kwa kila kilo; soma Kupunguza uzito kwa usalama.
Mazoezi – mmHg 4–8.
Pombe – wanaume vinywaji ≤2, wanawake ≤1 kwa siku, au acha.
Potassium – ndizi, parachichi, maharage, mboga za majani (isipokuwa kwa wenye ugonjwa wa figo).
Sigara – acha; huongeza hatari ya moyo hata presha ikidhibitiwa.
Kwa nini presha idhibitiwe
Kiharusi, shambulio la moyo, moyo kushindwa, figo kushindwa, upofu.
Mara nyingi haina dalili – soma Muuaji wa siri.
Nini cha kufanya
Pima presha nyumbani au famasia kila wiki mwanzoni.
Andika matokeo; mpelekee mtoa huduma.
Endelea na dawa ulizoandikiwa; mabadiliko ya maisha huweza kupunguza dozi baadaye kwa ushauri.
Lala vya kutosha; dhibiti msongo.
Dalili za hatari
Hospitali mara moja ukiwa na:
Presha 180/120 au zaidi pamoja na kichwa kikali, maumivu ya kifua, kushindwa kupumua, kuchanganyikiwa au uono kufifia.
Upande mmoja kulegea au kushindwa kuongea.
Lini umwone daktari
Presha 140/90 au zaidi mara mbili.
Presha haishuki baada ya miezi 3 ya mabadiliko.
Mjamzito mwenye presha ya juu.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
1. Naweza kushusha presha bila dawa?
Kwa presha ya juu kidogo, mara nyingi ndiyo; ya juu zaidi huhitaji dawa pia.
2. Chumvi kiasi gani?
Chini ya gramu 5 – kijiko kimoja cha chai kwa siku.
3. Mazoezi gani?
Kutembea haraka dakika 30, siku 5 kwa wiki.
4. Niache dawa nikianza mlo?
Hapana bila ushauri.
5. Kitunguu saumu kinasaidia?
Kidogo; hakichukui nafasi ya dawa.
6. Pombe inaongeza presha?
Ndiyo, ikinywewa nyingi.
Imeandikwa:
24 Agosti 2026, 03:58:17
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
World Health Organization. Guideline for the pharmacological treatment of hypertension in adults. Geneva: WHO; 2021.
Whelton PK, et al. 2017 ACC/AHA guideline for the prevention, detection, evaluation, and management of high blood pressure in adults. Hypertension. 2018;71(6):e13–115.
Appel LJ, et al. A clinical trial of the effects of dietary patterns on blood pressure (DASH). N Engl J Med. 1997;336(16):1117–24.
World Health Organization. Guideline: sodium intake for adults and children. Geneva: WHO; 2012.
Ministry of Health, United Republic of Tanzania. Standard Treatment Guidelines and National Essential Medicines List (STG/NEMLIT), 7th edition. Dodoma: Ministry of Health; 2026.

