Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
Dkt.Salome A, MD.
31 Oktoba 2026, 15:23:37

Maumivu ya tumbo kwa Mjamzito
Jibu kwa ufupi
Jibu kwa ufupi: Maumivu madogo yanayopungua ukipumzika – kawaida. Maumivu makali, damu, maji kutoka, homa, mikazo ya mara kwa mara kabla ya wiki 37, maumivu juu ya tumbo na kichwa kikali, au mtoto kupunguza kucheza – hospitali mara moja.
Maelezo
Kawaida
Mfuko wa uzazi kutanuka.
Round ligament – kuchoma pembeni ukijigeuza.
Gesi, choo kigumu, kiungulia.
Braxton Hicks – mikazo isiyo na mpangilio, hupungua ukipumzika.
Hatari
Miezi ya mwanzo – mimba nje ya kizazi, kuharibika; soma Mimba changa inayotoka damu.
UTI / figo – kuchoma kukojoa, homa, maumivu ya ubavu.
Kidole tumbo – kulia, homa, kutapika.
Uchungu wa mapema – mikazo ya mara kwa mara kabla ya wiki 37; soma Dalili za awali za uchungu.
Kondo kujitenga – maumivu makali yasiyokoma, tumbo gumu, damu.
Pre-eclampsia – juu kulia, kichwa, kuona ukungu; soma Kupima presha.
Kwa eneo
Chini – mfuko, kibofu, mishipa.
Upande mmoja – mishipa, mimba nje ya kizazi, figo, kidole tumbo.
Juu – kiungulia, nyongo, pre-eclampsia.
Nini cha kufanya
Pumzika, badilisha mkao, joto kidogo (si moto) mgongoni.
Maji, nyuzinyuzi; milo midogo.
Kojoa mara kwa mara.
Paracetamol kwa maumivu madogo; epuka NSAID kuanzia wiki 20.
Dalili za hatari
Hospitali mara moja ukiwa na:
Maumivu makali au yasiyokoma.
Damu ukeni, maji kutoka.
Homa, kutetemeka.
Mikazo 4+ kwa saa kabla ya wiki 37.
Kichwa kikali, kuona ukungu, maumivu juu ya tumbo.
Mtoto kupunguza kucheza.
Kizunguzungu, kuzimia.
Lini umwone daktari
Maumivu madogo yanayojirudia.
Kuchoma kukojoa.
Kukosa choo siku nyingi.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
1. Maumivu ya tumbo ujauzitoni ni kawaida?
Madogo ndiyo; makali – hospitali.
2. Kuchoma pembeni nikisimama?
Mara nyingi round ligament.
3. Mikazo isiyo na mpangilio?
Braxton Hicks; ikiwa ya mara kwa mara kabla ya wiki 37 – hospitali.
4. Maumivu juu kulia?
Huweza kuwa pre-eclampsia – pima presha leo.
5. Dawa gani?
Paracetamol; epuka NSAID kuanzia wiki 20.
6. Lini ni dharura?
Maumivu makali, damu, maji, homa, mtoto kupunguza kucheza.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 19:17:51
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
American College of Obstetricians and Gynecologists. Practice Bulletin No. 222: Gestational hypertension and preeclampsia. Obstet Gynecol. 2020;135(6):e237–60.
World Health Organization. WHO recommendations on antenatal care for a positive pregnancy experience. Geneva: WHO; 2016.
Cunningham FG, et al. Williams Obstetrics. 26th ed. New York: McGraw-Hill; 2022.
Ministry of Health, United Republic of Tanzania. Standard Treatment Guidelines and National Essential Medicines List (STG/NEMLIT), 7th edition. Dodoma: Ministry of Health; 2026.

