top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

Dkt. Salome A, MD

31 Oktoba 2026, 15:23:37

Oxytocin na Prolactin huongezeka kwenye damu baada ya kujifungua

Jibu kwa ufupi


Jibu kwa ufupi: Ni mabadiliko ya kawaida ya homoni yanayosaidia kunyonyesha na uhusiano na mtoto. Wenzi wakielewa na kusaidiana, mahusiano yao yanaimarika katika kipindi hiki.


Maelezo


Prolactin


  • Huchochea matiti kutengeneza maziwa.

  • Huwa juu sana siku za mwanzo, hushuka kidogo wiki 2 hadi 4, kisha hupanda kila mtoto anaponyonya.

  • Huongeza hamu ya mama kumtunza na kuwa karibu na mtoto.

  • Hupunguza estrojeni – uke mkavu na hamu ya tendo kupungua; soma Uke mkavu ukinyonyesha.


Oxytocin


  • Hukamua maziwa kutoka tezi hadi chuchu.

  • Husinyaza kizazi – soma Kunyonyesha husinyaza kizazi.

  • Huleta utulivu, hupunguza msongo, na huimarisha upendo kati ya mama na mtoto.


Athari kwa mahusiano


  • Mama anaweza kuwa na hamu ndogo ya tendo kwa miezi kadhaa – si kumkataa mwenzi.

  • Uchovu wa kumhudumia mtoto huchangia.

  • Mwenzi anayesaidia malezi na kazi za nyumbani huongeza ukaribu.


Nini cha kufanya


  • Zungumzeni wazi kuhusu hisia na mahitaji.

  • Mwenzi asaidie kumbeba mtoto, kazi za nyumbani na kumpa mama muda wa kupumzika.

  • Tafuteni ukaribu wa aina nyingine – kukumbatiana, mazungumzo.

  • Tumieni kilainishi tendo likirudi.

  • Soma Ngono baada ya kujifungua.


Dalili za hatari


  • Mama ana huzuni nyingi, anakosa usingizi hata mtoto akilala, au mawazo ya kujidhuru au kumdhuru mtoto – msaada mara moja.


Lini umwone daktari


  • Huzuni au wasiwasi zaidi ya wiki 2 baada ya kujifungua – sonona ya baada ya kujifungua.

  • Mahusiano yanaathirika sana – ushauri wa wanandoa.


Maswali yanayoulizwa mara kwa mara


1. Kwa nini sina hamu ya tendo baada ya kujifungua?

Prolactin na estrojeni ndogo, pamoja na uchovu – ni kawaida na hurudi taratibu.

2. Oxytocin inasaidia nini?

Kutoa maziwa, kusinyaza kizazi na kujenga upendo na mtoto.

3. Hamu ya tendo itarudi lini?

Kwa wengi taratibu ndani ya miezi michache, hasa kunyonyesha kukipungua.

4. Mwenzi wangu anajisikia kutengwa, tufanye nini?

Zungumzeni, shirikianeni katika malezi, tafuteni ukaribu wa aina nyingine.

5. Prolactin inazuia mimba?

Kunyonyesha pekee miezi 6 ya mwanzo kwa masharti maalumu kunaweza kuchelewesha mimba, lakini si kinga ya uhakika.

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 19:17:51

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

​

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

Rejea za mada hii:

  1. Uvnäs-Moberg K, et al. Maternal plasma levels of oxytocin during physiological childbirth – a systematic review. BMC Pregnancy Childbirth. 2019;19:285.

  2. Polomeno V. Sex and breastfeeding: an educational perspective. J Perinat Educ. 1999;8(1):29–42.

  3. Alder E, et al. The relationship between breastfeeding persistence, sexuality and mood in postpartum women. Br J Obstet Gynaecol. 1988;95(4):359–64.

bottom of page