Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
Dkt. Helen L, M.D
24 Agosti 2026, 03:43:15

Tabia ya kukufanya upate usingizi kwa wakati
Lala na amka muda uleule kila siku, zima taa kutengeneza giza na hakikisha hakuna kelele yoyote, zima na weka simu mbali na kitanda, usile mlo mkubwa wala kunywa kahawa au pombe masaa matatu kabla ya kulala na fanya mazoezi au kazi ya kukutoa jasho wakati wa mchana.
Hatua za kuzingatia ili upate usingizi kwa wakati
Tafiti zinaonyesha, kuna ongezeko kubwa la watu wenye madeni ya usingizi, hii inachangiwa na kukosa muda wa kulala unaoshauriwa kiafya. Madeni ya usingizi huchangia kupunguza ufanisi wa kimwili na kiakili.
Kujifunza namna nzuri ya kupata usingizi itasaidia kupunguza matatizo mengi yanayotokana na kukosa usingizi.
Mambo yafuatayo ili kupata usingizi kwa wakati
Lala na amka muda ule ule kila siku
Zima taa na hakikisha hakuna kelele sehemu unayolala kwa kuzima redio, TV n.k. Hakikisha pia wakati wa mchana unakuwa kwenye mwanga angavu.
Usinywe kahawa au kula mlo mkubwa wakati wa usiku haswa masaa matatu kabla hujalala
Usikae kwenye mwanga mkali au mwanga wenye rangi ya bluu wakati wa usiku
Usilale muda mrefu au bila mpangilio wakati wa mchana. Endapo unahitaji kulala wakati wa mchana hakikisha hulali zaidi ya lisaa moja au mawili
Ili kupata usingizi wakati unawaza vitu vingi, hesabu namba moja, mbili, tatu na kuendelea kwa kichwa bila kutamka mpaka utakapopata usingizi. Unaweza pia kufikiria kuhusu namna unavyovuta pumzi na kuitoa kutoka kwenye mfumo wa upumuaji
Tumia virutubisho au vyakula vinavyosemekana vinaleta usingizi
Pata tiba ya tatizo la msongo wa mawazo au magonjwa ya akili yanayosababisha kukosa usingizi
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 19:17:51
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
​
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
