Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
Dkt. Helen L, MD
Dkt. Sospeter B, MD
2 Aprili 2026, 19:17:51

Tangawizi kwa mjamzito
Chai ya tangaziwi imeonekana katika tafiti nyingi kuwa na uwezo wa kupunguza kichefuchefu na kutapika kwa wanawake wenye homa ya ujauzito inayofahamika pia kama homa ya asubuhi. Chai hii inaweza kutumika katika kipindi chote cha ujauzito isipokuwa kipindi cha kukaribu na uchungu au kwenye uchungu takribani wiki 2 hadi 3 za mwisho za ujauzito.
Wanawake wenye historia ya mimba kutoka kutokana na kutokwa damu wanashauriwa kutotumia chai hii ili kupunguza hatari ya mimba kutoka au kutokwa na damu katika ujauzito.
Kuna madhara kunywa tangawizi nyingi kwa mjamzito
Unywaji wa tangawizi nyingi kupita kiasi katika ujauzito huweza amsha uchungu na kutokwa na damu nyingi inayoweza kupelekea upungufu wa damu.
Hitimisho
Chai ya tangaziwi inayopunguza kichefuchefu na kutapika wakati wa ujauzito, haipaswi kutumika kipindi cha kuanza kwa uchungu ili kuzuia hatari ya kutokwa damu nyingi wakati huu na pia isitumike kwa wanawake wenye historia ya mimba kutoka na kutokwa na damu.
Wapi utapata maelezo Zaidi?
Kuhusu kiango gani cha tangawizi cha kutumia ili kudhibiti dalili za homa ya asubuhi, soma katika Makala nyingine ya chai ya tangawizi wakati wa ujauzito.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 19:17:51
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
